27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Tamwa yataka sheria kuwabana wazazi wasiolea watoto wao

Na Aziza Masoud -Kisarawe


CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wilayani hapa, kimeishauri Serikali kutunga sheria ndogo ndogo zitakazowabana wazazi wanaowapeleka watoto wao kulelewa kwa wazazi wao wazee kwa kuwa kufanya hivyo kunasababisha wengi wao kukosa huduma muhimu na uangalizi wa karibu zaidi.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike iliyofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Kazimzumbwi wilayani hapa juzi, Ofisa Ufuatiliaji Tathimini wa Tamwa, John Ambrose alisema ushauri huo ulitolewa katika kikao kilichoketi Septemba 18, mwaka huu na kuwajumuisha wadau hao.

Ambrose alisema lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili na kisha kutoa mapendekezo ya muda mfupi na mrefu kukabiliana na suala la unyanyasaji wa kijinsia.

Alisema miongoni mwa mapendekezo ya muda mrefu yaliyotolewa ni kuhitaji sheria hizo ndogo zitakazowabana wazazi kwa kuwa wanawarsha walibaini uwapo wa wimbi kubwa la watoto kutekelezwa vijijini na kulelewa na wazee yaani bibi au babu.

“Washiriki wa warsha walitoa mapendekezo ya muda mfupi na muda mrefu, miongoni mwa mapendekezo ya muda mrefu yaliyotolewa ni kuwapo kwa sheria ndogo ndogo za kuwabana wazazi wanaotelekeza watoto wao kwa wazazi wao wazee hali inayosababisha wengi wao kukosa huduma muhimu na uangalizi wa karibu,” alisema Ambrose.

Pia alisema wadau walitoa mapendekezo ya muda mfupi na washiriki waliona athari nyingi kwa watoto na wanawake zinachagizwa na ngoma za sherehe za usiku ‘vigodoro’ na unyago.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kisarawe, Mussa Gama alisema wanafunzi 16 wameripotiwa kupata mimba wakiwa shuleni kuanzia kipindi cha Januari hadi Septemba, mwaka huu na tayari wamechukuliwa hatua za kisheria.

“Takwimu zinaonesha watoto 25 walipata mimba mwaka jana… pia kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba, mwaka huu idadi ya mimba 16 zimeripotiwa na zilifikishwa polisi na mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria,” alisema Gama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles