27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

TAMTHILIA YA WILDFLOWER KUREJEA KWA KISHINDO NDANI YA STARTIMES SWAHILI

Ile Tamthilia yetu pendwa ya WildFlower msimu wa pili inarudi tena kwa Kishindo kuanzia tarehe 14 mwezi huu,itarushwa moja kwa moja na chaneli ya ST Swahili kuanzia saa 4:00 Usiku ,Jumatatu mpaka Ijumaa.


Tamthilia hii inamzungumzia mwanadada Lily Cruz amabaye anarejea Poblacion, Ardiente ili Kulipiza Kisasi cha wazazi wake ambao ni Dante na Calmia ambao waliuawa na familia ya Julia Adiente, hii yote ni katika kulipiza kisasi kwenye familia
Yakina Julio Ardiente.


Baada ya kunusurika kifo Lily akutana na mwanamke tajiri Prianka baada ya kufanikiwa kuachiwa na wauwaji,Prianka akamchikua Lily na kubadilisha kila kitu kuhusu Lily na kua na utambulisho mpya wa Ivy kama mtoto wake.Ivy alisomeshwa mpaka chuo kikuu na kua mtu mkubwa ,Prianka alimsaidia na kumfanya kua jasiri katika kila kitu na pia
alimsaidia kujua namna ya kupigania haki ya wazazi wake.


Baada ya Miaka 13 Ivy anagundua kua mama yake hakuuwawa,na baada ya msako mkali Ivy alifanikiwa kumuona mama yake,lakini mama yake matatizo ya kupoteza kumbukumbu ambapo Ivy alifanikiwa kumchukua na kumsadia kurudisha kumbukumbu zake.

Ivy alikua msichana machachari sana ,alifanikiwa kumteka kimapenzi kijana Arnado,Arnado akachanganyikiwa na penzi la Ivy lakini lengo la Ivy ilikua ni kuanika maovu ya Arnado na asiweze kuolewa nae..

Je ni Bomu gani jingine Ivy analiandaa????

Kaa tayari,Lipia kifurushi chako cha Uhuru kwa Tsh 18,000 tu ndani ya Startimes ufurahie uhondo wa Tamthilia hii

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles