27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

TAMMY THE BADDEST; UKIJITAMBUA HAKUNA WA KUKUOMBA RUSHWA YA NGONO

NA CHRISTOPHER MSEKENI


INALETA raha kuutazama muziki wa Bongo Fleva unaostawi ukiwa na ongezeko kubwa la jinsia ya kike, hususani wasichana walioamua kujikita kwenye muziki wa Kemo maarufu kama Hip Hop.


Ambao umejengwa kwa dhana ya kufanywa na wanamume zaidi kuliko wanawake hivyo anapoibuka msichana mwenye uwezo wa kuandika mashahiri makali, kufanya mitindo huru (Free Style) na kupita kwenye ile misingi ya muziki huo jamii inaanza kumtazama kwa jicho la kipekee.


Hasa ukizingatia wengi wao huvaa kiume, hutenda matendo ambayo huwa yanafanywa na wanamume kiasi kwamba kuna baadhi ya watu huanza kuwafikiria vibaya na wakati mwingine huwaingiza kwenye kashfa ya mapenzi ya jinsia moja (usagaji).


Hiyo ilikuwa ni kitambo lakini hivi sasa hali imebadilika, muziki wa rap una warembo ambao hufanana na wanamume kimichano na siyo kimwonekano, hakika wanavutia.


Wakati huu Bongo Fleva imejaaliwa kuwa na marapa wengi wakike tena wadogo kiumri ila wamekomaa kiuchanaji na wanaweza kukustaajabisha endapo ukiwapa nafasi ya kuburudisha hadhira.


Sikiliza kazi za rapa kama Chemical, Stosh, Pink, Cindy Rulz, Tammy na Rose Ree waliopachikwa jina la Dada Hood, hakina utakubaliana na mimi kuwa mabinti hawa wana sauti zenye mamlaka ya kuamrisha kichwa chako kitingishike kwa utamu wa mistari yao.


Juma3tata wiki hii lipo na mmoja ya warembo hao ambaye hivi sasa anasumbua mjini na ngoma yake inayoitwa Mtoto wa Kike, inachezwa kwa fujo kwenye redio na runinga zetu huyu ni Tamara Ally ‘Tammy The Baddest’.
Ni dada wa Hassan Kabunda
Tammy anasema katika familia yake wapo watoto watatu na yeye ndiye mtoto wa kwanza na ana wadogo zake wawili huku mmoja akiwa ni mcheza soka.


 “Mimi ndiyo dada  na nina wadogo zangu wawili ambapo anayenifuatia ni mchezaji wa Taifa Stars na Mwadui Fc anaitwa Hassan Kabunda ambaye ni mchezaji bora wa mwezi wa Februari,” anasema.

 

Godzilla alimshika mkono


Muziki ni kitu ambacho anakipenda muda mrefu na safari yake ramsi ya kuingia kwenye ulimwengu wa Hip Hop aliianza pale alipokutana na rapa Godzilla ambaye alimpeleka kwenye studio za Mj Records.


“Godzilla alinipeleka Mj Records na nikasainiwa na Master J, Marco Chali ambapo kupitia kundi la Young Chaliz tulifanya ngoma mbili tatu ambazo tuliwashirikisha Tunda Man na C Pwaa, hapo ndiyo watu wakaanza kunifahamu kama Tammy lakini kabla ya hapo nilifanya onyesho la ‘Free Style Star Look A Like’ ambalo tulikuwa tunafananishwa na baadhi ya mastaa wa nje,” anasema Tammy.

 

Hawezi kumsahau Ngwea


“Magwea ni kaka yangu kabisa, ni mtu ambaye alinivutia na alipenda kuniona kila siku nipo sehemu fulani, natamani angekuwepo ili aendelee kuona mafanikio yangu na yeye ndiyo alinipa jina la The Baddest sababu alikuwa anaamini ni mbaya wa kuandika mistari na floo,” anasema.


Mtazamo wake rushwa ya ngono

Moja ya sababu zilizopelekea muziki wa Bongo Fleva kuwa na wasichana wachache kuliko vidume ni kadhia ya kuombwa rushwa ya ngono na watayarishaji muziki, mameneja, watangazaji na mapromota, Tammy The Baddest analitazama vipi tatizo hili?
“Mimi sijawahi kuombwa rushwa ya ngono, unajua siku zote ukiwa wazi na kuonyesha kitu unachokitaka hakuna mtu yoyote kwenye tasnia anaweza akakushobokea na akaona mapenzi kwako ndiyo kila kitu, hakuna anayeweza kukuingilia na hizo swaga,” anasema.

 

Bado anapiga kazi na ‘We The Business’

Tammy anasema mipango ya kufanya kazi chini ya lebo ya We The Besiness iliyopo nchini Nigeria inaendelea na kikubwa ambacho kipo, ameambia aendelee kutafuta soko la Afrika Mashariki kwanza kabla hawajaachia kazi zilizopo chini ya lebo hiyo.
Jukwaa moja na Ludacris


Anasema kwenye historia ya muziki wake anajivunia kutumbuiza jukwaa moja na msanii mkubwa wa Hip Hop nchini Marekani, Ludacris mwaka 2011 katika tamasha la Fiesta, Dar es salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles