24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Tamisemi yaagiza wakuu wa shule kukamilisha ujenzi wa maabara

Mwandishi Wetu-Musoma

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Joseph Nyamhanga amewaagiza wakuu wa shule za sekondari kumalizia ujenzi wa maabara na uwekaji wa samani katika maabara hizo ili vifaa vilivyogawanywa na serikali katika shule hizo viweze kutumika kama ilivyokusudiwa.

Nyamhamga alitoa agizo hilo wilayani hapa jana, alipofanya ziara kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo zilizopo chini ya wizara yake.

Alisema Serikali iligawa vifaa vya maabara za sanyansi vyenye thamani ya zaidi yaSh bilioni 5 kwa shule 1,258 za sekondari kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo, lakini taarifa zinaonyesha vifaa vingi bado havijafungwa kwaajili ya matumizi na badala yake vimehifadhiwa ndani ya maboksi.

Alisema kwa mujibu wa taarifa hiyo, maabara nyingi bado hazijakamilika hususan samani zake hivyo kuwataka wakuu wa shule kwa kushirikiana na bodi za shule kuhakikisha maabara zinakamilika wakati huu wa likizo na vifaa kuwekwa tayari kwaajil ya mafunzo shule zitakapofunguliwa.

Alisema lengo la Serikali la kununua vifaa,ni kuhakikisha  wanafunzi wanakuwa na vifaa sahihi kwa ajili ya kujifunzia, jambo ambalo alisema litasiadia uelewa wa wanafunzi katika masomo ya sayansi na itachangia pia ongezeko la wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi.

Alisema vifaa hivyo ambavyo vilismabazwa katika shule hizo mwishoni mwa  waka jana na mwanzoni mwa mwaka huu, vinatakiwa kutumika na si kuhifadhiwa katika maboksi jambo ambalo alisema kuwa kwa kufanya hivyo linawanyima fursa wanafunzi kujifunza kwa vitendo na kwamba pia utunzaji huo sio salama kwa vifaa hivyo.

Alisema Serikali bado ipo mchakato wa kuboresha elimu katika shule za umma ili watoto waweze kujifunza na kuongeza ufaulu wao hasa katika masomo ya sanyansi na kwamba katika mwaka huu wa fedha,Serikali inatarajia kujenga maabara katika shule saba za sekondari katika kila halmashauri nchini.

Wakizungumzia uboreshaji huo,baadhi  ya wakazi wa Wilaya ya Tarime, waliiomba Serikali uboreshaji huo uende sambamba na ongezeko la idadi ya walimu wa masomo ya sayansi katika shule za umma.

Walisema nia  ya Serikali itazaa matunda endapo kutakuwepo na walimu wa kutosha wa masomo ya sayansi kuliko ilivyo sasa ambapo walimu wa masomo hayo  ni wachache mno.

Pendo Wambura alisema  shule nyingi za sekondari za umma hazina kabisa walimu na kwa zile ambazo wana walimu basi idadi ya walimu inakuwa ni upungufu kuliko.mahitaji hivyo maabara hizo zikijengwa na vifaa kusambazwa suala la walimu pia linapaswa kuzingatiwa.

” Unakuta shule nzima kuna mwalimu mmoja wa sayansi au hakuna kabisa sasa ili.maabara hizo ziwe na manufaa kwa wanafunzi, Serikali iajiri walimu wa sayansi watakao wafundisha wanafunzi kwa vitebdo kuliko sasa ambapo walimu hao hawapo,” alisema Matiko Nyasaricho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles