27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Tamisemi kujenga Nyumba ya walimu Sekondari ya Lumuma, Mpwapwa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imeahidi kujenga Nyumba ya walimu two in one itakayojengwa kwa kupitia mradi wa EP4R katika shule ya sekondari Lumuma yenye madarasa sita ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu (Mb), George akikagua ujenzi wa miundo mbinu ya madarasa katika shule ya sekondari Lumuma jimbo la Kibakwe Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa.

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, George Simbachawene alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara na wananchi wa kata Lumuma baada ya kujionea maendeleo ya ujenzi wa shule  hiyo.

“Gharama za matofali katika ujenzi wa nyumba hiyo ya walimu zitatolewa na nguvu kazi ya wananchi na tunaweza kujenga nyumba mbili za aina hiyo kama tutakaza msuli vizuri.

“Kupitia fedha za mfuko wa jimbo nitasaidia katika kukamilisha ujenzi wa miundombinu mingine, ikiwa ni pamoja na kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala,” amesema Simbachawene.

Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene ameelekeza Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa kusajili barabara ambazo hazijasajiliwa hasa zinazoenda kwenye maeneo ya huduma za kijamii au maeneo mapya ya utawala ambayo yameongezeka.

Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene akikagua ujenzi wa shimo la choo katika sekondari ya Lumuma jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

“Halmashauri inapaswa kuzifungua na kisha kuzisajili kwa mujibu wa mchakato wa kisheria, ambapo lazima kamati ya maendeleo ya kata ikae na kuzibainisha baraba mahali zilipo na urefu wake na kuonesha taasisi inayokwenda ili kupeleka mapendekezo kwenye halmashauri na baadae kupeleka DCC kisha kwenye bodi ya barabara ya mkoa (Road Board).

“Barabara hizi zikisajiliwa kwa mujibu wa sheria ni rahisi kwa TARURA kuzitambua na kuzitengea fedha,” amesema Simbachawene.

Awali, katika taarifa yake Diwani wa Kata ya Lumuma, Joktan Chelligah amesema wananchi wa kata ya Lumuma wamejenga shule hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja.

“Wananchi tumechanga fedha kiasi cha Sh million 17, lakini halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa imetuchangia Sh million 20, na mifuko 150 ya saruji pamoja na mabati 250, na Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dodoma kimechangia mifuko 130 ya saruji,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles