23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TAMASHA LA KUSAFIRI UTUPU LILIVYOSISIMUA ABIRIA ULAYA

Untitled-1JUMAPILI iliyopita wasafiri wanaotumia treni mijini walijionea makubwa wakati wenzao walipovua suruali au sketi zao na kubaki na chupi pekee katika mataifa mbalimbali ya Ulaya na Amerika.

Hali hiyo ilitokana na tamasha la ‘kusafiri bila chupi’ ambazo huandaliwa katika miji tofauti ya nchi za magharibi kila mwaka tangu mwaka 2002.

Hufanyika kila Januari, ambapo tarehe hubadilika mwaka hadi mwaka zikiwa zinatangazwa mapema Desemba.

Awali tamasha hili lilianza kama kundi dogo la vijana saba na limezidi kukua na kugeuka kuwa la kimataifa kusherehekea kile kinachoitwa upuuzi!

Wakati wa hafla hiyo, wazo ni kuwataka abiria wanaopanda treni za chini ya ardhi mijini katika vituo tofauti kusafiri kama wasafiri wa kawaida wakati wa majira ya baridi bila chupi.

Washiriki hufanya kana kwamba hawafahamiani na wote huvaa makoti ya baridi, kofia, skafu na glovu, lakini kitu pekee cha kushangaza ni kutovaa suruali au sketi.

Na hilo hulifanya baada ya kupewa ishara ya kuvua mavazi yao hayo ya chini kwa pamoja na kubaki na chupi pekee.

Mmoja wa waandalizi wa hafla hiyo jijini New York Jesse Good alinukuliwa akisema: “Tunataka kuwapa wakazi wa New York fursa ya kuinua macho kutoka kwa magazeti yao na simu zao ili angalau wajionee kitu tofauti na kile walichozoea kuona kila siku.”

Licha ya hali ya joto kufikia nyuzi sifuri huku kukiwa na baridi na upepo mkali, wakazi wa New York nchini Marekani hawakujali hilo walijitosa wakiwa na vichupi katika tamasha hilo lililofanyika Jumapil iliyopita.

Wakiwa wamevalia kofia, skafu na makoti mazito, walipanda treni katika vituo mbalimbali huku wakiwa katikati ya wasafiri waliokuwa katika mshangao.

Miji mingine ambako hafla hizo ziliandaliwa ni Boston pia Marekani, Berlin nchini Ujerumani, Prague nchini Jamhuri ya Czech na Warsaw nchini Poland, Mexico City nchini Mexico, Bucharest, Romania, Milan nchini  Italia.

Wao huhitajika ‘kuvaa sura ya kazi’ hata wanapojibu maswali wanayoulizwa na wengine kama vile; ‘je wanahisi baridi?.

Mmoja wa wahusika, Peter Saez alinukuliwa akisema: “Watu ambao hawaelewi tunachofanya watatutazama kana kwamba tunafanya makosa.”

Naye Toni Carter akasema: “Si kawaida kwangu kupata nafasi ya kuvua nguo zangu mbele ya umati na kujionyesha nilivyoumbwa nikaumbika. Ninatumbuiza jiji la New York. Kwangu, hii ni Sanaa.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles