Tamasha la kuibua vipaji kufanyika Mwanza

0
1458

MBASHA FROLANA GEORGE KAYALA

TAMASHA kubwa la kuibua waimbaji wa nyimbo za injili limepangwa kufanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Mkurugenzi Mtendaji wa tamasha hilo, Fabian Fanuel, alisema tamasha hilo pia litatumika kupinga mauaji ya
watu wenye ulemavu wa ngozi.

“Tamasha hilo litaanza Mwanza, kisha mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa, lengo likiwa ni kupinga mauaji ya albino, lakini pia kuibua na kukuza vipaji vipya vya waimbaji wa nyimbo za injili,” alisema Fanuel.

Katika tamasha hilo, waimbaji maarufu wa muziki wa injili wataongozwa na Flora Mbasha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here