TAMAA YA FEDHA ITAKAVYOMTOKEA PUANI MAYWEATHER

0
817

ADAM MKWEPU NA MITANDAO

BONDIA wa uzito wa kati, Floyd  Mayweather ni bondia ambae hakawii kubadili uamuzi wake linapokuja suala  la dau la  fedha nyingi kwani yupo tayari kupigana bila kuangalia  anapigana nani ilmradi fedha inaingia.

Ni muda mrefu tangu Mayweather aseme  anaachana na ndondi lakini hivi karibuni amekubali kurudi ulingoni kuzichapa na Conor McGregor.

Litakuwa pambano kati ya bondia bora na bondia mwenye jina kubwa katika mchezo wa ngumi mchanganyiko.

Pambano kati ya Mayweather na Conor McGregor limekuwa likizungumziwa sana japo kuna wakati ilionekana kama  halitatokea lakini hatimaye muafaka umepatikana  na sasa watapanda ulingoni Agost 26 mwaka huu mjini Las Gas, Marekani.

Pambano hilo litachezwa chini ya sheria za mchezo wa Boxer japokuwa McGregor hajawahi pigana mchezo huo popote pale lakini yeye ni mchezaji wa ngumi mchanganyiko  tu hivyo itamalazima kuzingatia sheria za mchezo huo.

Kwa kigezo hicho cha sheria kitakuwa kikimpa faida zaidi Mayweather ambaye una uzoefu wa muda mrefu wa kutumia sheria hizo, kuliko mpinzania wake.

Hata hivyo pambano hilo la uzani wa Middleweight litakuwa lenye thamani kubwa duniani katika historia ya masumbwi.

Mayweather, ambaye ni bingwa wa zamani katika mizani mitano tofauti na ambaye anajulikana kuwa bondia bora wa kizazi chake alistaafu mwaka 2015 baada ya mapigano 49 bila kushindwa.

Mmarekani huyo aliwahi kutetea taji lake la WBC na WBA, mafanikio ambayo yalimwezesha kuifikia rekodi iliowekwa na Rocky Marciano ya mapigano 49.

Mayweather alistaafu kwa mara ya kwanza 2008 baada ya mapigano 39 kabla ya kurejea tena ulingoni.

McGregor ambaye hajawahi kupigana ndondi za kulipwa alifanikiwa kuwa bingwa wa UFC Novemba mwaka 2016, amekuwa akiomba kupigana na Mayweather chini ya sheria za pigano linaloshirikisha ngumi mchanganyiko.

Mayweather ataweka mfukoni kiasi kikubwa cha fedha ambacho tayari wachambuzi wa masuala ya masumbwi wameshaanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu  muda aliokaa nje anaweza kupigwa.

Bondia huyo tangu Septemba mwaka 2015 hakuwahi kupata pambano baada ya kudundana na bondia Andre Berto.

Wapo wanaojiuliza kwanini pambano hilo limetokea sasa? Jibu ni kwamba  kila bondia ameahidiwa kupata kiasi cha dola milioni 100 ambayo sawa na pauni milioni 78.

Ni fedha nyingi na huenda likavunja recodi nyingi za mapambano yaliyopita kwa kuwa pambano lenye thamani kubwa zaidi kutokea duniani.

Baada ya Mayweather kushinda kwa pointi dhidi ya Andre Berto Septemba mwaka  2015, bondia huyo alisema: “Kazi yangu imekwisha rasmi kuanzia sasa.

“Unatakiwa kutambua muda mzuri wa kucheza ulingoni, hakuna nilichobakisha kuthibitisha katika ndondi, nahitaji kutumia muda na familia yangu.”

Hata hivyo baada ya kutupiana maneno ya kejeli kwa muda mrefu, McGregor akidai : “Naweza kumfanya Mayweather kuwa taahila ndani ya ulingo.”

Mkurugenzi Mtendaji wa matangazo ya Maywether, Leonard Ellerbe, alisema: “Hakuna sehemu ambayo tulikwenda na Mayweather mashabiki wasiulize kuhusu pambano lake na McGregor, kwa sasa Mayweather anafikiri kuhusu kushinda pambano hilo.”

Rais wa mchezo wa ngumi za mchanganyika, Dana White anaamini aina ya upigaji wa McGregor unaweza kumpa wakati mgumu Mayweather.

“Mayweather ana umri wa miaka 40 na akiwa ulingoni ana tatizo la kushindwa kuwamudu mabondia wanaotumia mkono wa kushoto.

“McGregor ana miaka 28 na anatumia zaidi mkono wa kushoto kurusha konde lake na likikupata lazima udondoke chini,” anasema White.

Ulingo wa T-Mobile Arena unachukua watu 20,000 hivyo pambano hilo litafanyika robo ya mashabiki 90,000 ambao walifurika kumshuhudia Bingwa  wa uzito wa juu Duniani, Anthony Joshua alipopigana na Wladimir Klitschko katika ulingo wa Wembley April mwaka huu.

Fedha katika pambano hilo hazitapatika katika mageti tu bali zipo njia nyingi baadhi ni haki za matangazo za televisheni za kimataifa na wadhamini.

Makamu Rais wa kituo cha televisheni cha Showtime Sports, Stephen Espinoza, anasema mashabiki watalipa kutazama pambano hilo kwasababu ya umaarufu wa wahusika.

“Hakuna cha kufananisha, hakuna bondia aliyepigana aina hii ya pambano, hatuwafuati mashabiki wa dondi na ngumi za mchanganyiko bali tunawataka mashabiki ambao hawafuatilii mchezo wa ngumi,”anasema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here