UONGOZI wa Taliban umewataka raia wa Afghanistan wanaoingia barabarani kuacha mara moja, la sivyo watapata wanachokitafuta.
Kauli ya Taliban imetanguliwa na hatua yake ya kutumia silaha za moto kutawanya maelfu ya waandamanaji jijini Kabul.
Katika video zilizosambaa mitandaoni, waandamanaji wanaopaza sauti kutaka Kundi hilo liheshimu haki za wanawake wanaonekana wakikimbia, huku milio ya risasi ikirindima.
Mbali ya haki za wanawake, waandamanaji wamesikika wakiionya Pakistan kwa madai kuwa nchi hiyo jirani imekuwa ikilisaidia Kundi la Taliban.