23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

TALGWU YAWATAKA WAKURUGENZI KUFUATA SHERIA ZA UTUMISHI

Na Asha Bani, Dar es Salaam

Chama cha Wafanyakazi Wa Serikali za Mitaa (TALGWU), kimewataka Wakurugenzi nchini kufanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria na haki za watumishi Wa umma.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne Aprili 10, jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wa TALGWU, Rashid Mtima alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya kurudishwa kazini kwa wafanyakazi walioishia darasa la saba.

Amesema yalifanyika makosa na wakurugenzi kwa kutofuata utaratibu ambapo baadhi ya watumishi wapatao 7,382 waliondolewa kazini kimakosa.

“Katika idadi ya wafanyakazi hao 3,504 walikuwa ni wanachama wa TALGWU jambo ambalo liliwaathiri kwa kiasi kikubwa,” amesema.

Aidha, ameipongeza serikali kwa kuwasikiliza pindi walipokuwa wakiwahitaji kwa ajili ya vikao na hatimaye juzi kutoa uamuzi huo wa kuwarudisha kazini.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles