27.7 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Talaka itanikuta kwenye shughuli zangu- Mke wa Dk. Mwaka

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Di

Aliyekuwa Mke wa Dk. Juma Mwaka, anayefahamika kama Queen Oscar amesema kuwa ameamua kujiweka kando na masuala yanayohusiana na ndoa yake nakwamba kama ni talaka itamkuta kwenye shughuli zake.

Queen ameyasema hayo Dar es Salaam leo Machi 20, 2023 muda mchache baada ya kusaini mkataba wa ubalozi wa kampuni ya uagizaji na uuzaji magari ya BM Car Dealers Co Ltd.

Amesema kwa sasa bado hajapata talaka kutoka kwa mume wake Dk. Mwaka nakwamba muda mwingi anautumia kwa ajili ya kuwatafutia ridhiki watoto wake.

“Licha ya Dk. Mwaka kutokunipa talaka mpaka sasa, nimeamua kuendelea na maisha yangu kwa ajili ya kuwatafutia ridhiki watoto wangu na talaka itanikuta kwenye shughuli zangu, ninayo furaha kubwa kuwa napata nafasi ya kuwa balozi na kuwa mfanyakazi katika kampuni ya BM Car Dealers Co. LTD namshukuru Mungu kwa ukuu wake maishani mwangu,” amesema Queen.

Pia amesema kuwa alitamani kupata nafasi ya kuwa balozi wa kitofauti katika jamii pamoja na yote ambayo amepitia ila Mungu amemshika mkono kwani hawezi kuwasahau Watanzania wenzake ambao alilia nao pamoja..

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo, John Mwakalonge amesema wanayo furaha kwa kumpata mwanamke ambaye ana weledi mkubwa katika sekta ya biashara kwani ataleta mchango mkubwa katika kampuni yao.

“Queen ni mwanamke mwenye uwezo mkubwa katika sekta ya biashara na sisi kama BM Car Dealers Co. LTD tunayo furaha kufanya kazi naye,” amesema Mwakalonge.

Pia ameongeza kuwa wao wamejikita katika uagizaji wa magari na kuuza ndani na nje ya nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles