Takukuru yamuhoji mkurugenzi wa zamani Hai

0
725

MWANDISHI WETU – KILIMANJARO

TAASISI ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Takukuru inamhoji aliyekuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Hai, Johari Baleli kwa tuhuma ya upotevu wa jumla ya Sh milioni 300 zilizolengwa kujengea kituo cha afya Hai.

Kwamujibu wa Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kilimanjaro, Fedels Kalungula ni kwamba Mkurugenzi huyo anahojiwa kutokana na kiasi hicho cha fedha kutofahamika kilipo licha ya kutolewa na serikali.

Alieleza kuwa hali hiyo imetokana na kusimama kwa ujenzi wa kituo hicho cha afya bila sababu za msingi na kwamba katika ufuatiliaji ikabainika kutumika nje ya lengo lililokusudiwa na serikali.

Kalungula alisema hali hiyo imetokana na taarifa za upotevu wa fedha hizo ambazo zilitolewa kwa ajiri ya kuondoa kero ya wananchi lakini hata hivyo kituo hicho hakikujengwa na hakukuwa na taarifa zozote za kutokamilika kwa mradi huo.

“Serikali ilitoa kiasi cha Shilingi milioni 300 kwa ajili ya  kujenga kituo cha afya lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika na tulianza kufuatilia na tukakosa taarifa sahihi za zilipo fedha hizo na ndipo tukaamua kumhoji aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo,” alisema 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here