20.5 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Takukuru yamshikilia mwalimu kwa kufanya udanganyifu kwenye mitihani

Mohamed Hamad-Manyara

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru Wilayani Kiteto mkoani Manyara, wanamshikilia mwalimu mkuu wa shule ya msingi Orkitikiti, Kijiji cha Engong’ongare wilayani humo, Oscar Waluye kwa tuhuma ya kufanya udanganyifu wa mitihani ya darasa la saba inayoendelea kufanyika hapa nchini.

Makungu alisema mtuhumiwa huyo akiwa ni mwalimu mkuu wa shule hiyo aliwalazimisha wanafunzi wawili wa darasa la sita katika shule hiyo kufanya mtihani ya darasa la saba, badala ya mtahiniwa ambao uwezo wao darasani unaelezwa kuwa ni wa kiwango cha chini.

Alisema mwalimu huyo pia anatuhumiwa kukaririsha mwanafunzi na kuwaingiza kwenye chumba cha mtihani wanafunzi wawili wa darasa la sita pamoja na mwanafunzi aliyehitimu shule mwaka jana kufanya mtihani huo ulioanza jana.

Kamanda Mkungu alisema baada ya kupata taarifa hizo, walifika shuleni hapo na kuwakuta wanafunzi hao wakiwa wameshafanya mitihani ya masomo ya kiswahili na hesabu kinyume cha sheria na hivyo kuwatumia wanafunzi wasiostahili kufanya mitihani hiyo.

Alidai kuwa wanafunzi hao mamluki walikuwa wanafanya mtihani hiyo kwa niaba ya wenzao wa darasa la saba ambao wanadaiwa kuwa na uwezo mdogo huku aliyekaririshwa akitumia jina la mwanafunzi mtoro shuleni hapo.

Kamanda Holle alisema uchunguzi unaendelea na utakapokamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mwalimu huyo ambapo alitoa wito kwa walimu kufanya kazi kwa uadilifu kulea watoto katika njia ipasayo ikiwa ni pamoja na kusoma kwa bidii badala ya kufanya udanganyifu katika mitihani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles