29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

TAKUKURU YAMSAKA PAUL CHRISTIAN

Na MWANDISHI WETU -TABORA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  (Takukuru) mkoani Tabora, inamsaka mwandishi na mtangazaji wa Redio Sauti ya Tabora (Voice of Tabora), Paul Pele Christian kwa siku kadhaa sasa bila mafanikio.

Habari  za uhakika ambazo MTANZANIA imezipata mjini hapa, zinasema amekuwa akisakwa na maofisa wa taasisi hiyo kwa mahojiano kuhusu kashfa inayomuhusisha na sakata la vyeti vya elimu anavyodaiwa kuvitumia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kujiendeleza kielimu.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tabora, Fidelis Kalungula, aliliambia MTANZANIA kuwa wanamtafua Christian kwa siku kadhaa sasa, lakini hawajafanikiwa kumpata.

“Kweli tunamtafuta kwa mahojiano, hatujafanikiwa kuonana naye,” alisema Kalungula bila kufafanua zaidi.

Akizungumza kwa simu na MTANZANIA, Christian alikiri kupigiwa simu na maofisa wa taasiisi hiyo wakimtaka afike ofisini kwao kwa mahojiano.

“Nimepigiwa simu na maofisa wa Takukuru nifike ofisini kwao, leo (jana) ni siku ya nne sijatokea,” alisema.

Christian alisema kila anapohitajika amekuwa akibanwa na majukumu mengi ya kazi zake, hivyo kushindwa kuwajibu lolote akihofia kuwapotezea muda wao.

Alisema hii si mara ya kwanza kuhojiwa na maofisa wa taasisi hiyo, kwani walishafanya hivyo mara mbili.

Christian alisema mara ya kwanza ilikuwa Aprili 15, mwaka huu alipopigiwa simu na Kaimu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tabora, akidai ana mazungumzo naye.

Alisema baada ya wito huo, alifika ofisi za Takukuru saa 8:20 mchana.

“Katika mazungumzo yetu, walitaka kujua historia niliposemea kuanzia elimu ya msingi, sekondari, chuo na namfahamu vipi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,” alisema.

Alisema mara ya pili alihojiwa tena Mei 10, mwaka huu saa 5 asubuhi kwa muda wa saa tatu.

“Mbali ya mahojiano na maofisa hao, niliwakabidhi nakala za vyeti vyangu vya elimu ya sekondari,” alisema.

Pia alisema Mei 15, mwaka huu, alipata taarifa ya kutafutwa tena na taasisi hiyo kwa mahojiano kupitia kwa mkurugenzi wake wa Voice of Tabora, Ismail Aden Rage.

Christian alisema kuwa anashangazwa na hatua ya kutafutwa mara kwa mara, japo mhusika wa suala hilo yuko Dar es Salaam.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles