25.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Takukuru yampandisha ofisa afya kizimbani

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma, imemfikisha mahakamani Ofisa Afya Mkuu Msaidizi wa Wilaya ya Kongwa, Anania Madono (57) kwa kosa la kupokea rushwa ya Sh 200,000 ili asiyakamate madumu 63 yenye lita 309 za mafuta ya alizeti  kwa kisingizio kwamba  hayakuwa na vifungashio.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini hapa jana, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sostenes Kibwengo alisema uchunguzi umeonyesha kuwa, mwanzoni mwa Novemba mwaka huu, mshitakiwa alikamata na kushikilia madumu 63 yenye lita 309 za mafuta ya alizeti kwa madai kuwa hayakuwa na vifungashio na alimtaka mmiliki ampe fedha hizo ili amuachie.

Kibwengo alisema mtuhumiwa huyo alipokea rushwa Novemba 8 mwaka huu eneo la Kibaigwa wilayani Kongwa na kurejesha madumu hayo kwa mmiliki baada ya kupokea fedha hizo.

Kibwengo alisema pia Takukuru imemfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma Elibariki mngahani (29 ) ambaye ni Ofisa Uhamiaji na kumfungulia mashitaka mawili ya kushawishi na kupokea rushwa ya 500,000 kinyume na kifungu cha 15(1)cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.

“Uchunguzi wetu umeonesha kwamba  Oktoba 3 mwaka huu majira ya saa 5 usiku  katika eneo la Dodoma Hotel mshitakiwa alishawishi na kupokea rushwa hiyo kutoka kwa Saulabh Tanwar kama kishawishi ili imsaidie kuachiwa kwa Gange Thangadurai, raia wa India, ambaye alikuwa ameshikiliwa na maofisa wenzake wa uhamiaji kwa kosa la kuwazuia kufanya kazi yao,” alisema.

Katika hatua nyingine, Kibwengo alisema Mahakama ya Wilaya ya Bahi imetoa uamuzi wa shauri la jinai namba 46/2019 la kumhukumu Daudi Masigati, Mjumbe wa Baraza  la Ardhi Kata ya Chikole aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka mawili ya kushawishi na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15(1) cha Sheria  ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2017.

Alisema mahakama imemtaka mtuhumiwa kulipa faini ya Sh. 500,000 au kwenda jela kwa miaka mitatu kwa kila shtaka.

“Uamuzi huo ulitolewa baada ya mahakama kuridhishwa na ushahidi uliowasilishwa na Takukuru  kufuatilia uchunguzi ulionyesha kwamba mwaka jana alishawishi na kupokea rushwa ya Sh. 200,000 ili amsaidie mtoa taarifa wetu kushinda shauri lake la mgogoro wa ardhi lililokuwa linaendelea kwenye Baraza,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles