29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

TAKUKURU YAINGILIA KATI PEMBEJEO ZA KILIMO

Na AMON MTEGA- SONGEA


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Ruvuma, itaanza kutoa ushauri wa namna ya kugawa pembejeo za kilimo kwa wakulima mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mbeya, Yustina Chagaka, alisema ofisi yake imejipanga kutoa ushauri huo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wakulima.

Kwa mujibu wa Chagaka, wananchi walioleta malalamiko hayo walisema wamekuwa wakikosa pembejeo hizo za ruzuku kila mwaka bila kuwapo sababu za msingi.

Alisema kwamba, utaratibu unaolalamikiwa unaonyesha kuna mazingira ya rushwa, kwa kuwa wanaonufaika na mpango huo wa Serikali, wamekuwa ni wale wale kila mwaka.

“Kutokana na uwepo wa malalamiko hayo, sisi kama taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa tumeamua kuyavalia njuga malalamiko hayo ili haki iweze kutendeka.

“Kwa maana hiyo, tutatoa ushauri kwa wahusika ili tuhakikishe haki inatendeka wakati wa kugawa pembejeo hizo, kwani wanaozihitaji ni wengi,” alisema.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,682FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles