27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Takukuru yabaini udhaifu Ruwasa Simiyu

Na Derick Milon, Simiyu

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Simiyu (TAKUKURU) imesema kuwa imebaini kuwepo kwa madhaifu kwenye miradi 8 ya maji ambayo inatekelezwa na Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoani humo.

Madhaifu hayo yamebainika wakati Takukuru ikifanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma katika utekelezaji na usimamizi wa miradi hiyo yenye thamani ya sh. Bilioni 6.4 ikiwemo miradi miwili ya elimu katika kipindi cha julai hadi septemba 2020.

Hayo yamesemwa leo mbele za waandishi wa habari na Kamanda wa Takukuru Mkoa Joshua Msuya wakati akitoa taarifa ya shughuli zilizotekelezwa na taasisi hiyo kipindi cha julai hadi septemba 2020 ofisini kwake mjini Bariadi.

Kamanda Msuya amesema kuwa walibaini kuwa miradi yote ya maji imechelewa kuanza utekelezaji na ukamilishaji kinyume na maelekezo ya miongozo na mikataba ya utekelezaji wake.

Amesema kuwa licha ya Ruwasa Simiyu kupokea fedha za kutekeleza miradi hiyo mapema sana kutoka serikalini, baadhi ya miradi ilianza kutekelezwa mwezi juni, 2020 ikiwa ni miezi nane tangu wamepokea fedha hizo.

Madhaifu mengine ni kuwepo kwa ucheleweshaji wa vifaa vya ujenzi katika miradi na ucheleweshaji wa malipo kwa mafundi uliofanywa na Ruwasa Mkoa, ikiwa pamoja na kuchelewa kuunda bodi ya wazabuni.

Hata hivyo Msuya amesema kuwa Ruwasa walijitetea kuwa madhaifu hayo yanatokana na wao kusubilia mwongozo kutoka makao makuu, jambo ambalo alisema utetezi huo haukuwa na ukweli kwani fedha zilikuja na miongozo moja kwa moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles