27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

TAKUKURU YAANZA UCHUNGUZI TPA

Na PATRICIA KIMELEMETA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) imeanza kuchunguza magari yote yaliyokwama katika ya Bandari Tanzania(TPA) yakiwa yameagizwa kwa majina ya taasisi za serikali.

Akizungumza na MTANZANIA jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Takukuru, Musa Misalaba alisema agizo la Rais Dk. John Magufuli linahitaji utekelezaji wa haraka ili kuwabaini wahusika wa magari hayo na kwa nini waliamua kutumia taasisi za Serikali ikiwamo Ofisi ya Rais kuyaingiza.

Alisema kwa sababu Rais Dk. Magufuli ametoa siku saba za utekelezaji wa agizo lake, ufuatiliaji ulianza mara moja na inategemewa utakamilika katika muda uliopangwa.

“Tumepewa siku saba na Rais Dk. Magufuli kuhakikisha tunachunguza magari haya na kuwasilisha ripoti, hivyo basi tulianza kazi baada ya kutolewa kwa agizo, tunaamani kazi itakamilika kwa muda uliopangwa ili tuweze kuwasilisha taarifa,” alisema Misalaba.

Alisema uchunguza utahusu mambo mengi hivyo unahitajika umakini ili kuhakikisha wahusika wanapatikana.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. aliyeweka sahihi, aliyelipia nje, ni nani.Ebu CCM acheni mchezo mchafu. Mkitaka kumjua mtamjua tu. Kuna malipo yamefanyika nje. Jina gani na benki gani pesa zimetoka. Nyinyi muwadanganye Watanzania wasiojua na wanawashangilia. Mtu mzima mwenye elimu safi atawashangaa kila mnaposema hamumjui aliyeleta. Mkipiga simu huko magari yanatoka wanabili, na risiti za malipo, oda na sahihi, benki iliyotuma pesa. Hawa Wasomi wanaokimbilia CCM wote ni wasomi wanaotafuta vyeo tu. Wako pamoja na chama chao kuendeleza udanganyifu, ufisadi na kuwadhurumu watu wachini. Hata kama huna elimu, jiulize, huwezi kupata gari kwenye makampuni bila malipo, bila kuweka sahihi, bila kupata risiti. Na risiti zinatunzwa na mtumaji na kopi inawekwa kwenye mzigo. Mnaoitetea CCM na mnaona wazi bado uwongo unaendelea, wizi, na kuwaweka ndani wapinzani. Bado mnaiamini. Faida za elimu zenu ni nini? Watanzania Wasomi wote mnashindwa kuwa wakweli. Mnashindwa kuwa mashujaa. Mnashindwa kuwasaidia maskini.Mnazinyonga suti barabarani badala ya kuwa na heshima, hadhi, na fikra.Bado mnakuwa vibaraka bila aibu. Hizi dini zilizozagaa Tanzania zinashindwa kuwasaidia Watanzania. AIBU GANI>

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles