24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Takukuru wamdaka anayedaiwa kumtapeli DC Jokate Kisarawe

MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

TAASISI ya ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nchini imemkamata Omari Chuma (55) anayedaiwa kumtapeli Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo baada ya kujifanya ofisa wa Serikali.

Mkazi huyo wa Chamazi wilayani Temeke, Dar es Salaam, anayedaiwa kutenda kosa hilo Wilaya ya Kisarawe jana, alitarajiwa kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Pwani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi wa taasisi hiyo, Ali Mfuru, alisema Chuma alikamatwa na maofisa wa Takukuru baada ya kupokea taarifa kutoka Kisarawe.

“Tumefanikiwa kumkamata ikiwa ni takribani wiki tatu tangu Takukuru iutangazie umma kuhusu kukamatwa kwa matapeli wengine sita walioshirikiana kufanya utapeli. Kati ya watuhumiwa hao, wanne walijifanya ni maofisa wa Takukuru wa vyombo vingine vya dola na wawili walitoka katika kampuni ya simu,” alisema Mfuru.

Alisema uchunguzi umebaini matapeli hao wana mtandao unaohusisha wafanyakazi wa ofisi mbalimbali zikiwemo za Serikali na wamekuwa wakifuatilia watumishi na viongozi na kujifanya ni maofisa wa Takukuru.

“Uchunguzi wetu umebaini kuwa matapeli hawa wana mtandao unaojumuisha watu kutoka maeneo na ofisi mbalimbali zikiwemo za Serikali na wamekuwa wakiwafuatilia watumishi au viongozi ambao kwa njia moja au nyingine wanaweza kuwa na tuhuma na hivyo kuwadai fedha (rushwa) huku wakijifanya wao ni maofisa wa Takukuru,” alisema Mfuru.

Alisema Chuma mwenye umri wa miaka 55, alikamatwa na maofisa wa Takukuru baada ya kupokea taarifa kuwa mtuhumiwa huyo alifika katika Ofisi za Jokate kwa nia ya kumtapeli kwa kujifanya kuwa yeye ni Ofisa wa Serikali kutoka Ikulu.

“Baada ya kupokea taarifa hizi pamoja na taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali, Takukuru ilianzisha uchunguzi dhidi ya mtuhumiwa huyu na kuthibitisha makosa chini ya sheria zifuatazo ikiwemo Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007: i Kujifanya Afisa wa Serikali kinyume na kifungu Na 100 (b) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code) Sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002, ii.

Kuomba, kushawishi au kujaribu kujipatia au kujipatia rushwa kinyume na kifungu Na. 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na 11/2007,” alisema Mfuru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles