30.3 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Takukuru: Wajumbe ardhi wapewe elimu

AMON MTEGA- RUVUMA.

MKUU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Ruvuma, Yustina Chagaka ameitaka idara  inayoshughulika na masuala ya ardhi mkoani humo kutoa elimu ya mara kwa mara kwa wajumbe waliopo katika mabaraza ya ardhi ili kupunguza malalamiko.

Wito huo umetolewa jana na mkuu huyo ofisini kwake, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji ya robo mwaka kwa waandishi wa habari.

Alisema idara ya ardhi, inaongoza kulalamikiwa na wananchi mbalimbali  na kumekuwapo viashiria vya mianya ya rushwa.

Alisema utendaji kazi wa robo ya mwaka, kumekuwapo na malalamiko mengi yanatoka sekta ya ardhi ambayo hadi sasa yamefika 17.

Alisema migogoro inayoshughulikiwa na mabaraza ardhi ya vijiji na kata,wajumbe wake wengi wameteuliwa kushughulikia migogoro hiyo huku hawana elimu ya utambuzi kuhusu masuala ya ardhi.

Alisema baadhi ya wajumbe, wanatumia nafasi hiyo kujipatia vipato kwa walalamikaji kwa kuwaambia watoe gharama za kwenda maeneo ya migogoro  ambako mwisho wa siku anayetoa kiasi kikubwa ndiye anayeonekana mwenyewe haki.

“Ofisi yangu imepata malalamiko mengi kutoka idara hii, tumejipanga kupambana nalo kisawasawa…haiwezekani migogoro imekuwa mingi mno eneo hiuli,”alisema Chagaka.

Alisema idara zingine zinazolalamikiwa na idadi ya malalamiko katika mabano, ni elimu (10), halmashauri (7),Serikali za mitaa (5), polisi (5),vyama vya ushirika (4), mahakama (4), maji (3) na taasisi za fedha (2). Kuhusu miradi ya maji, alisema kwa  asilimia kubwa imekuwa na matatizo kukamilika

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles