22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Takukuru Simiyu yaokoa zaidi ya milioni 100 za NDC, AGITF

Na Derick Milton, Simiyu

Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa mkoa wa Simiyu (TAKUKURU) mkoa wa Simiyu imefanikisha kurejeshwa kwa zaidi ya shilingi Milioni 117 zilizokopwa na wakulima kutoka Mfuko wa Pembejeo za kilimo (AGITF) pamoja na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC).

Fedha hizo zinatokana na mikopo ya matrekta ambayo wakulima 11 wa mkoa wa Simiyu walikopa kutoka mfuko wa pembejeo Sh milioni 700,800,000, huku wakulima wengine 9 wakikopa Sh milioni 112,000,000 kutoka NDC.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo leo kwa waandishi wa habari kipindi cha Januari hadi Machi 2021, Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa Alex Mpemba amesema kuwa wakulima hao walikopa pembejeo hizo katika kipindi cha mwaka 2003 hadi 2008 na mwaka 2018.

Mpemba amesema kuwa wakulima hao baada ya kukopa Pembejeo mbalimbali yakiwemo matrekta, walishindwa kurejesha kwa muda ambao waliingia makubaliano na NDC pamoja na Mfuko wa Pembejeo za kilimo (AGITF).

Alisema kuwa wakulima waliokopa mfuko wa pembejeo, wamerejesha kiasi cha Sh milioni 104,800,000 kati ya milioni 700,800,000 walizokopa, huku waliokopa NDC wakirejesha milioni 12,500,000 kati ya Sh 122,000,000 walizokopa.

“Mfuko wa Pembejeo pamoja na NDC baada ya kuona wateja wao wameshindwa kurejesha mikopo hiyo kwa muda mrefu, walituomba Takukuru kuwasaidia kufuatilia madeni hayo, ambayo yameanza kurejeshwa,” amesema Mpemba.

Taasisi hiyo imesema kuwa wanaendelea kuwafuatilia wakulima wote ambao bado hawajarejesha mikopo hiyo, ili kuweza kurejeshwa kwa kaisi chote ambacho walikopa kutoka kwenye taasisi hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,280FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles