25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

TAKUKURU Simiyu yakuna kichwa Rushwa ya Ngono

Na Derick Milton, Simiyu

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Simiyu imesema kuna changamoto kubwa sana ya kuripoti matukio ya rushwa ya ngono kutoka kwa wahusika au watendewa matukio hayo.

Aidha, imesema kuwa wengi wa watendewa wa matukio hayo wanakosa ujasiri, huku kukiwepo na usiri mkubwa wa watu kuweza kutoa taarifa katika ofisi zao au kwenye mamlaka nyingine kwa ajili ya kuchukua hatua.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Simiyu, Janeth Machulya.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 11, na Mkuu wa Takukuru Mkoa, Janeth Machulya wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, ambapo ameeleza kuwa taasisi hiyo imeanza kutafuta njia za kupambana na matukio hayo.

Machulya amesema kuwa licha ya ofisi yake kutopokea taarifa hata moja ya rushwa ya Ngono, bado kumekuwepo na taarifa za pembeni za matukio hayo ambazo wamekuwa wakizisikia kutoka kwa wananchi mbalimbali.

Amesema kuwa katika kupambana na hilo, hivi karibuni waliandaa warsha na wadau wa elimu mkoa, ambapo walichambua mifumo ya viashiria vya rushwa na kuazimia kuundwa kwa madawati ya rushwa ya ngono kwa ajili ya kuripoti matukio hayo.

“Katika warsha hiyo ambayo tuliwakutanisha wadau wote wa elimu, eneo ambalo limekuwa na tatizo hilo, tulikubaliana kuundwa kwa madawati hayo ambayo yataanzishwa kwenye maeneo yao ya kazi huko huko,” amesema Machulya.

Aidha, Mkuu huyo wa TAKUKURU amesema kuwa kupitia madawati hayo wahusika wa matukio hayo wataweza kutoa taarifa na kama watashindwa basi wataelekezwa ni wapi sehemu salama wanaweza kutoa taarifa zao.

“Jambo ambalo tumeligundua ni kuwa rushwa ya ngono kuigundua ni kazi ngumu sana, kwani kuna usiri mkubwa sana lakini pia wengi hawana ujasiri wa kuripoti haya matukio, ndiyo tukaja na hiyo njia ya madawati ambayo watu wanaweza kuyatumia kutoa taarifa,” amesema Machulya.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Takukuru amesema kuwa taasisi hiyo katika utekelezaji wa shughuli zake za kila siku, katika kipindi cha Januari hadi Machi, 2022 wameweza kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ameeleza katika utekelezaji wa zoezi hilo katika kipindi hicho, wameweza kukagua miradi mbalimbali ya barabara iliyoko chini ya TARURA na mapungufu ambayo walibaini TARURA imeweza kuyafayia kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles