21.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

TAKUKURU Simiyu yabaini madudu mifuko ya jimbo

Derick Milton, Simiyu

TAASISI ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Simiyu imebaini ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu katika matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo kwenye majimbo ya Meatu, Itilima, Bariadi na Busega mkoani humo.

Hayo yamebainishwa leo na Kamanda mkuu wa taasisi hiyo Mkoa, Adili Elinipenda wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa ofisi yake kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi, 2019 kwa waandishi wa habari ofisini kwake.

Elinipenda amesema taasisi hiyo ilibaini kuwa mfuko wa jimbo kwenye majimbo hayo, fedha zake zimekuwa zikitumika pasipo kuhidhinishwa na kamati ya mfuko wa jimbo husika kama ilivyoelekezwa katika sheria.

“ Sheria ya fedha za kuchochea maendeleo ya mfuko wa jimbo namba 16 ya mwaka 2009 (The Constituencies Development Catalyst Fund Act of 2009) inatoa mwongoza wa jinsi gani fedha hizo zitumike lakini majimbo haya hayafuati sheria hii,” amesema.

Elinipenda amesema wahusika kwenye mfuko huo wanatakiwa kutambua sheria iliyowekwa kuendesha fedha hizo, ni lazima kufuatwa na wala siyo hiari ya mtu au baadhi ya watu kufanya wao wanavyotaka.

“ Wengine wanasema wanaamua kutumia busara, kwenye fedha za umma hakuna busara hata kidogo, fedha hizi zimeletwa kwa ajili ya maendeleo kwa hiyo ni lazima sheria zake zifuatwe, kama taasisi tutakaa na wahusika kuwaeleza hilo jambo,” amesisitiza Kamanda huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,580FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles