Takukuru kuwahoji Maofisa sita Jeshi la Zimamoto

0
723

Ramadhan Hassan, Dodoma

Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Makubaliano Kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Kampuni ya Rom Solution Company Ltd ya nchini Romania wanatarajia kuhojiwa leo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) jijini Dodoma.

Wajumbe hao sita wameitwa katika mahojiano hayo wakiwa na laptop walizopewa na Kampuni ya Rom Solution.

Kwa mujibu wa Takukuru wanaohojiwa leo ni Kamishna wa Zimamoto, Mbaraka Semwanza, Naibu Kamishna wa Zimamoto, Fikiri Salala, Naibu Kamishna wa Zamamoto, Lusekela Chaula, Naibu Kamishna wa Zimamoto, Ully Mburuko, Ofisa Ugavi Mkuu wa Zimamoto, Boniface Kipomela na Mchumi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Felis Mshana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here