23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

TAKUKURU Kagera yaweka vipaumbele kwa kufuatilia miradi

Na Renatha Kipaka, Kagera

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Kagera imeweka vipaumbele vya utekelezaji wa majukumu kwa kipindi cha Oktoba na Desemba, mwaka huu kwa kufanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo.

Akizungumza na na Waandishi wa Habari mjini Bukoba leo Jumatano Oktoba 6, Mkuu wa TAKUKURU mkoani hapa, John Joseph amesema wameweka vipaumbele hivyo kwa lengo la kuongeza uhakiki wa thamani ya fedha inayotolewa na Serikali ili iweze kuonekana.

Amesema kumekuwa na malalamiko mbalimbali kuhusiana na vitendo vya rushwa, ufujaji mali za ushirika, makusanyo ya fedha za ndani kwenye Halmashauri kupitia  mfumo wa kieletroniki (POs), afya, michezo na asilimia 10 ya fedha inayotegwa na serikali kwa ajili ya Vijana, Wanawake na wenye ulemavu.

“Serikali imekuwa ikitoa fedha za utekelezaji wa miradi ambapo kwa kumbukumbu  ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoisema Septemba 27, mwaka huu Dodoma katika kikao cha ALAT, alisema kuwa:

“Bado kuna shida kwenye thamani ya fedha kwa miradi mnayoitekeleza, fedha nyingi zinakuja kwenu lakini miradi haifanani na fedha, naagiza thamani ya fedha katika miradi tunayoitekeleza ionekane” lengo letu ni kuziba mianya ya rushwa na upotevu wa raslimali katika utekelezaji wa miradi na kuwa na kiwango kinachotakiwa kulingana na thamani inayotolewa.”amesema Joseph.

Ameongeza kuwa kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Julai hadi Septemba, mwaka huu zimefanyika tafiti tano kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera ikiwa ni katika nyanja za mbalimbali.

“Utafiti wetu ulilenga katika kuthibitisha thamani ya Sh bilioni 4.18 katika miradi hiyo ambayo imetumika katika ujenzi wa hospitali na zahanati, ukarabati wa miradi ya maji, pamoja na ujenzi wa madarasa,”amesema Joseph.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles