24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 28, 2023

Contact us: [email protected]

TAKUKURU Kagera yataja vipaumbele vya kudhibiti rushwa

Na Renatha Kipaka, Kagera

Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera imetaja vipaumbele vyake kwa kipindi cha Junuari hadi Machi, 2023 vinavyolenga kudhibiti Rushwa isitokee.

Hayo yamebainishwa juzi na Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera, Ezekie Sinkala wakati akitoa taarifa ya utekelezaji ya miezi mitatu.

Sinkala amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni kuendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuziba mianya ya ufujaji wa fedha za umma.

Amesema kipaumbele kingine ni kuongeza kasi ya uelimishaji umma kwa kutumia njia mbalimbali na kutatua kero mbalimbali katika jamii kupitia program ya Takukuru Rafiki .

Pia amesema kuwa jambo jingine ni kufanya chambuzi za mifumo hasa katika maeneo yanayolalamikiwa zaidi na wananchi ili kuboresha na hatimaye kuondoa mianya ya rushwa itokanayo na mifumo ya utendaji .

Aidha, kwa kipindi cha miezi mitatu Sinkala ameongeza kuwa wamepokea jumla ya malalamiko 90 kati ya malalamikohayo malalamiko 65 yalikuwa ni malalamiko yasiyohusu rushwa ambapo walalamikaji walielimishwa na kupewa ushauri na hakukuwa na taarifa iliyohamishiwa idara nyingine .

Malalamiko 25 yalihusu rushwa na kufunguliwa majarada ya uchunguzi kati ya majarada 25, uchunguzi wa majarada 11 umekamilika na hatua za kisheria zinatarajiwa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa na majarada 14 uchunguzi wake bado unaendelea.

Amesema idara zinazolalamikiwa kutokana na taarifa 90 ni Halmashauri 45 idara ya fedha 9, Iiara ya elimu 4, maendeleo ya jamii 2, ugavi 5, maji
2, idara ya afya 6, watendaji wa kata na vijiji 4.

Taarifa zingine 13 zilihusu watu binafsi 2, tasisi za kifedha 2, Mashirika binafsi (NGO) 2, polis 2, Mahakama 2, na TANESCO 3

Sinkala ameongeza kuwa mashauri mapya 9 yalifunguliwa mahakamani na kufanya jumla ya mashauri 34 yanayondelea kusikilizwa mkoani Kagera.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,224FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles