‘Taifa linahitaji maridhiano ya kisiasa’

0
660
RAIS wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS), Omar Said Shaaban
RAIS wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS), Omar Said Shaaban
RAIS wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS), Omar Said Shaaban

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

RAIS wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS), Omar Said Shaaban, amesema  hatua ya kuwepo kwa mkwamo wa kisiasa katika pande zote za Muungano ni vema yakafanyika maridhiano ya kisiasa nchini.

Alisema mbali ya hali ya kisiasa visiwani Zanzibar pamoja na uwepo wa mgawanyiko wa wazi miongoni mwa wananchi kuhusu Katiba inayopendekezwa inatosha kuwa sababu ya kutafuta maridhiano ya kitaifa juu ya rasimu ya Katiba na wapi pa kuanzia.

Kauli hiyo aliitoa juzi jijini Dar es Salaam, alipokuwa akiwasilisha mada katika Mkutano wa Kidemokrasia wa Chama cha ACT-Wazalendo, ambapo pia mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania(JUKATA), Deus Kibamba na Ababu Namwamba ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Labour cha nchini Kenya walitoa mada juu ya michakato ya Katiba na wapi nchi za Afrika zilipokwama.

“Pamoja na kugawanyika kwao kwa kiasi kikubwa hasa kutokana na itikadi za kisiasa, Wazanzibari waliunganishwa na matarajio kuwa Zanzibar itaendelea kuwepo na Tanzania itaendelea kuwepo.

“Hakuna Mzanzibari alikuwa ana matarajio Zanzibar kupotea kabisa baada ya mchakato wa Katiba lakini sasa hali hii inaanza kutoweka”alisema.

Alisema msingi wowote wa kuendelea kusigina katiba katika visiwa vya Zanzibar kunaendelea kusogeza mbali dalili za maridhiano miongoni mwa wananchi.

“Marekebisho ya kumi na mmoja yalifanywa hivi karibuni ambapo Ibara ya 66 ya Katiba inayotaka Rais ashauriane na Kiongozi wa Upinzani ndani ya Barza La Wawakilishi na kama hayupo basi chama kingine chenye Uwakilishi barazani hivi sasa kimerekebishwa na hakilazimishi chama chenye Uwakilishi ndani ya baraza bali chama chochote cha Siasa,” alisema Omar Shaaban

Aliongeza kuwa ni   muhimu kuzingatia na kukumbuka kuwa Mabadiliko ya 8, 9 na ya 10 yalichangiwa sana na matokeo ya misigano ya kisiasa Visiwani Zanzibar na kushuhudiwa ile iyokuwa  inaitwa Miafaka ya kisiasa ya mwaka 1999, 2001na 2005 na Maridhiano ya mwaka 2009

Alisema mara  kadhaa Zanzibar imeshuhudia  viongozi wa Serikali walioapa kuilinda Katiba wakiwa vinara wa kuikiuka ambapo alitolea mfano mwaka 1997, Zanzibar chini ya Utawala wa Dk. Salmin Amour Juma,  ilipopitisha  Sheria ya Bandari kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kipengele cha 11  inayotaja Bandari kama jambo la Muungano

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here