23.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

TAFIRI yaja na mfumo wa kidigitali kuunganisha sekta ya uvuvi

Na Esther Mnyika, Dodoma

Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) imesema imekuja na mfumo wa kidigitali ambao utarahisisha uvuvi na utaunganisha wavuvi, wauzaji, wachuuzi na watumiaji wa bidhaa za samaki.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Agosti 2, 2024 jijini Dodoma Afisa Utafiti TAFIRI, Spohia Shaban kwenye maonesho ya Wakulima nanenane kitaifa hufanyika jijini humo alisema duniani imabadilika kila kitu ni kiganjani wameanzisha app ambayo itawasaidia wavuvi.

Alisema mfumo huo wa kiteknolojia utasaidia wavuvi katika shughuli zao na kupewa elimu jinsi ya kutumia na umezinduliwa rasmi mwaka jana.

“Lengo la kuanzisha mfumo wa kidigitali ni kurahisisha huduma kwa wavuvi kupatikana kwa urahisi samaki na dagaa na mvuvi lazima awe na simu janja ajue kusoma na kuandika ili aweze kuingia kwenye app akiwanavyo tayari atapewa vifaa ikiwemo Global position system (GPS),”alisema.

Alisema kupunguza gharama za mafuta kupitia mfumo huo unaweza kujua leo samaki wanapatikana wapi kwa kiasi gani na soko gani lina samaki wa aina gani.

Sophia alisema kwa sasa mfumo huo wameanza na ukanda wa bahari na app inafanya vizuri na lazima uwe na leseni ya samaki unaowavua na chombo ambacho anatumia.

“Kwa wafanyabiashara, kwaajii ya kula majumbani samaki nao wanaweza kuingia kwenye app kuangalia leo kuna samaki feri au wavuvi gani wanasamaki kwasababu taarifa zao za msingi unapata kwenye mfumo,” aliongeza.

Aidha alisema wanaendelea kutoa elimu kwa wavuvi na wadau mbalimbali kutumia na mfumo huo ili wapate bidhaa za samaki kwa urahisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles