24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

TAEC yasisitiza uombaji vibali kidijitali

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
 
Wadau na wafanyabiashara nchini wamesisitizwa kupata vibali vya vipimo vya mionzi vinavyotolewa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa mfumo wa kieletroniki wanapoingiza na kusafirisha bidhaa ndani na nje ya nchi.
 
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Idara ya Ufundi na Kinga ya Mionzi wa TAEC, Yesaya Sungita kuhusiana na utoaji wa vibali hivyo unaofanyika sasa kwa njia ya mtandao.
 
Utoaji wa vibali hivyo kwa njia ya mtandao umeanza Aprili Mosu mwaka huu ambapo kwa sasa wadau na wafanyabiashara wanapaswa kuwasilisha maombi yao ya vibali kwa kutumia mtandao uitwao rac.taec.go.tz  ambapo mteja atapaswa kujaza fomu kwa njia ya mtandao na kuwasilisha kwa ajili ya kupata vibali.
 
“Tang u tumeanza mfumo huu wa utoaji vibali, umesaidia sana kurahisisha kazi na kupunguza mzigo kwa wateja au kupoteza muda ambapo kwasasa ndani ya saa mbili hadi nne baada ya kulipia na kuwasilisha sampuli mteja anaweza kupata kibali chake tofauti na zamani ambapo ilikuwa ikichukua takribani siku moja hadi tatu kwa mteja kupata kibali.
 
“Kubwa kwa wateja wanapaswa kujaza taarifa zenye usahihi ambazo hazitaleta mkanganyiko wakati wataalamu wanaotoa vibali watakavyopitia kabla ya kuidhinisha kwenye mtandao,” amesemaSungita.
 
Pamoja na mambo mengine, amesema awali iliwalazimu wafanyabishara kutumia muda mwingi kufika katika ofisi za TAEC kwa ajili ya kuwasilisha nyaraka zao na sampuli za bidhaa na kwamba sasa urahisi umepatikana nakuongeza tija katika utoaji wa vibali na kwamba umeondoa usumbufu kwa wadau katika upatakanaji wa vibali hivyo.
 
Sungita amesema kwa kutumia mfumo huu mteja atapaswa kuomba kibali moja kwa moja kupitia katika mfumo na kupewa gharama stahili na kuwa baada ya malipo kukamilika mteja ataweza kupata kibali chake kupitia mfumo huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles