TAEC yasaini mkataba ujenzi maabara ya kisasa

0
569
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Profesa Lazaro Busagala akibadilishana mkataba wa muendelezo wa ujenzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa maabara ya TAEC, wenye thamani ya Sh bilioni 10,474 na Mkurugenzi wa Kampuni ya M/S Li Jun Development Construction Ltd. Maabara hiyo itajengwa kwenye Makao Makuu ya TAEC yaliyopo Njiro, jijini Arusha.

Mwandishi Wetu, Arusha

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), iko mbioni kuanza ujenzi wa awamu ya pili ya maabara kisasa itakayojengwa na Kampuni ya Ujenzi ya M/S Li Jun Development Construction Ltd.

Tayari tume hiyo imesaini mkataba wa Sh bilioni 10.474 kwa ujenzi wa maabara hiyo itakayojengwa kwenye Makao Makuu ya TAEC, yaliyopo Njiro jijini Arusha.

Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Profesa Lazaro Busagala ameitaka kampuni hiyo kuhakikisha inajenga maabara hiyo kwa kiwango cha hali ya juu kulingana na makubaliano ya mkataba husika.

“Maabara hii ni mwendelezo wa maabara ya awamu ya kwanza iliyozinduliwa Aprili  mwaka huu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na pia ujenzi huu ni juhudi nyingine za serikali katika kuendelea kuleta maendeleo nchini,” amesema Profesa Busagala.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here