24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

TAEC kuzifunda kampuni za simu, watumiaji wa mionzi usalama wa wafanyakazi, mazingira

Mwandishi Wetu, Arusha

Kampuni mbalimbali za simu, taasisi na watafiti nchini zinazohusika na vyanzo vya mionzi isiyoayonisha (Non Inonizing Radiation) wakiwamo watumiaji wa vifaa tiba (MRI&Ultra sound) wametakiwa kutembelea Makao Makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) katika Kitengo cha Udhibiti wa Mionzi kwa lengo la kujifunza na kupata kupata ujuzi utakaosaidia kulinda usalama wa wafanyakazi, wananchi na mazingira dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi hiyo.

Ofisa Mtafiti wa vifaa vya nyuklia, Idara ya Mionzi isiyoayonisha, Injinia Christina Nyaki amesema kwa kufanya hivyo kutasaidia kuboresha ulinzi na usalama mahala pa kazi kwa wafanyakazi, wananchi na mazingira kuhusiana  na mionzi ya aina hiyo nchini.

“Tunatoa wito wa watafiti na makampuni kuja kupata ujuzi utakaowasaidia kujilinda ili kuwa salama katika maeneo yao ya kazi kwa lengo la kulinda watu na mazingira.

“Sheria Namba 7 ya mwaka 2003 ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, inawapa mamlaka ya kusimamia na kukagua maeneo mbalimbali yenye mionzi isiyoayonisha kama vile kwenye minara ya simu, vituo vya usambazaji wa masafa ya utangazaji, vituo vya rada, katika laini kubwa za usambazaji wa umeme na katika vifaa tiba,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema Tanzania iko chini ya Kamati ya Kimataifa ya Udhibiti wa Mionzi Isiyoanisha, International Committee for Non-ionizing radiation (ICNIRP) inawataka kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa watoa huduma za namna hiyo ili kujiridhisha wote wenye kutumia vifaa hivyo nchini kama wanakidhi vigezo husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,476FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles