26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

TAEC kutoa elimu ya nyuklia Nanenane

Mwandishi Wetu

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), itatoa elimu kwa wananchi watakaohudhuria Maonesho ya Nanene kuhusu masuala mbalimbali ikiwamo jinsi  teknolojia ya nyuklia inavyotumika katika sekta mbalimbali nchini.

Maonesho hayo yanayoanza leo Jumamosi Agosti Mosi, yatafanyika katika Viwanja vya Maonesho TASO mkoani Arusha kwa mikoa ya Kanda ya Kaskazini huku kitaifa yakifanyika kwenye Viwanja vya Nyakabindi, Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TAEC, Peter Ngamilo amesema teknolojia ya nyuklia inatumika katika sekta ya maji, mifugo, kilimo, viwanda na migodi, hivyo ni fursa ya pekee kuhudhuria katika viwanja hivyo ili kupata elimu juu ya matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia hapa nchini.

Maonesho hayo yamezinduliwa leo kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi na Makamu wa Rais , Samia Suluhu Hassan na yatafungwa na  Rais Dk. John Magufuli siku ya kilele Agosti 8, mwaka huu.

Kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020“.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles