24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Tacaids kushirikiana na Wasafi kutoa elimu ya VVU

Anna Potinus – Dar es Saaam

Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), wametangaza kushirikiana na kampuni ya Wasafi Ltd katika kupeleka ujumbe kwa jamii kuhusiana na suala la afya kupitia tamasha la Wasafi festival ambapo wasanii watapata fursa ya kutoa elimu kwa vijana juu ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Julai 10, katika ofisi za Tacaids zilizopo Posta jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa kampuni ya Wasafi na mwanamuziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul maarufu ‘Diamond Platnumz’, amesema lengo kuu la ushirikiano huo ni kuangalia ni namna gani wasanii wanaweza kutumia vipaji vyao kuelimisha jamii.

“Tuliona tuandae tamasha la Wasafi festival ambalo litatukutanisha na kutumia sanaa yetu katika njia zilizo sahihi hivyo tukaona sasa imefikia muda kutumia ushawishi tulionao na katika kulifanikisha hilo tukasema tukishirikiana na Tacaids pengine tutafikisha ujumbe mzuri zaidi,” amesema.

“Hauwezi kutimiza ndoto zako kama hauna afya bora hivyo tukiwa kama wasanii ambao Mungu ametupa Baraka za ushawishi tunaweza tukafikisha ujumbe kwa wenzetu wakatuelewa hivyo tumeshirikiana na Tacaids katika kuwaelimisha vijana namna ya kutumianafasi tulizonazo katika njia chanya zitakazoleta maendeleo katika nchi yetu,” amesema.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Tacaids, Jumanne Issango, amesema vijana ndio kipaumbele katika katika mapambano dhidi ya ukimwi na kwamba ndio kundi lenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya virusi vya ukimwi

“Utafiti uliofanyika 2016/17 unaonyesha kwamba maambukizi ya virusi vya ukimwi katika kundi la vijana kati ya miaka 15-24 wanachangia asilimi 40 ya maambukizi mapya kati ya maambukizi ya idadi ya watu 72,000 kitaifa kwa mwaka hivyo baada ya kuzindua utafiti huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa agizo kwa Tume kutumia wasanii kufikisha ujumbe na elimu ya VVU na Ukimwi na kuhamasisha suala la upimaji kwa vijana,” amesema Issango.

“Majukwaa ya wasanii ni mengi lakini mwaka huu tumebahatika kushirikiana na Wasafi tumeambiwa takribani wasanii 20 wana ushawishi hivyo tumeona ni fursa nzuri katika kuwafikishia ujumbe vijana juu ya maambuziki ya virusi vya ukimwi, eneo muhimu ambalo tutaliwekea msisitizo ni pamoja na matumizi ya Condom, upimaji na sasa hivi vijana wako katika mtandao kwahiyo tutahakikisha tunatumia akaunti za wasanii hawa kupitishia jumbe,” amesema Issango.

Aidha Issango amesema kupitia tamasha hilo wanatarajia kuwafikia vijana milioni 15 na kutakuwa na utoaji wa elimu, ugawaji wa condom na vipeperushi vitakavyokuwa na maelezo juu ya maambukizi hayo ambapo ametoa wito kwa wasanii wengine kufuata mfano wa wasafi wa kutoa elimu juu ya maambikizi ya ukimwi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles