25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Tacaids: Jitihada zinahitajika kuimarisha vyanzo vya ndani kupambana na UKIMWI

Na Nadhifa Omary, Singida

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko amesema jitihada za ziada zinahitajika katika kuimarisha vyanzo vya ndani vya fedha za kupambana UKIMWI nchini.

Baadhi ya Waratibu wa Ukimwi kutoka Wizara, Mikoa na Halmashauri walioshiriki katika kikao cha usambazaji wa taarifa ya mapitio ya fedha za UKIMWI kwenye sekta za umma na sekta binafsi ya mwaka 2022

Akizungumza Februari 22, 2023 wakati wa kufunga kikao cha waratibu wa UKIMWI kutoka Wizara, Mikoa na Halmashauri kilichofanyika mkoani Singida cha usambazaji wa taarifa ya mapitio ya fedha za UKIMWI kwenye sekta za umma na sekta binafsi ya mwaka 2022.

Dk. Maboko alisema fedha za UKIMWI zinazidi kupungua kwa asilimia 15 mwaka hadi mwaka, hivyo kuwa jitihada za ziada zinahitajika katika kuimarisha vyanzo vya ndani.

Hadi sasa fedha nyingi zinategemewa katika Mwitikio wa UKIMWI ni zile zinazotoka kwa wadau wa maendeleo bado hatujafikia pazuri katika vyanzo vyetu vya ndani (domestic financing) na hata fedha inayopangwa katika lengo A katika bajeti ya Mwaka katika Wizara na taasisi za Umma haipatikani ili kutekeleza Malengo yaliyokusudiwa.

Changamoto ni kuwa kama nchi bado hatujaweza kujitegemea wenyewe katika Mwitikio wa VVU na UKIMWI, licha ya malengo yaliyopo ya kufikia 2030 kuwa kama nchi tuwe tumefikia sifuri tatu, maambukizi mapya sifuri, vifo viwe vimefikia sifuri na unyanyapaa uwe umefikia sifuri.

Sehemu ya washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

Dk. Maboko alisisitiza kuwa ni kweli kuwa fedha kutoka kwa wafadhili zinapungua katika miaka miaka 2 hadi mitatu ya nyuma na mwelekeo wa wa miaka ijayo kupitia vikoa vya watalaamu na wadau wa maendeleo fedha za mwitikio wa VVU na UKIMWI zinaendelelea kupungua kwa silimia 15.

Aidha wakati wa kongamano la kimataifa la UKIMWI lililofanyika nchini Canada Mkurugenzi wa UNAIDS Duniani alisema katika miaka 3-5 ijayo  mabilioni ya fedha za UKIMWI zitapungua na hili sio suala  la Tanzania pekee ni changamoto ya nchi zote.

“Sasa lazima tuimarishe vyanzo vya fedha za ndani,kwani malengo yapo pale pale na hatujayafikia na maambukizi mapya kwa mwaka watu 54,000 wanapata maambukizi ya VVU, hii ukichukulia kwa siku watu 147 wanapata maambukizi mapya, ambapo mwaka 2007 watu 200 walikuwa wanapata maambukizi mapya.

“Takwimu zinaonesha kwamba asilimia 30 ni kwa vijana wa miaka 15 hadi 24, ambapo kwa siku vijana 44 wanapata maambukizi ya VVU, wakati huo takwimu zinaonesha vijana wa kike 31 wanapata maambukizi ya VVU kwa siku kupitia takwimu hizi ni wazi kuwa kuna haja ya kuweka nguvu na raslimali nyingi kwa vijana.

Sehemu ya Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

“Miradi ya vijana kwa kutegemea wafadhili yaani PEPFAR tupo katika halamshauri 11 lakini kwenye mipango ya mwaka huu zitafika halmashuri 14 kupitia mradi wa Dreams, wakati Global fund ni halmashauri 18 zilizofikiwa kwahiyo hadi sasa ni halmashauri 32 kati ya halmashauri 187,” amesema Maboko.

Pamoja na upungufu uliopo bado hatujafikia halmashauri zote nchini kwahiyo ni muhimu, tunapopanga mipango yetu vipaumbele viwe kwa maeneo ambayo hayajafiwa na wafadhili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles