NA LUCAS RAPHAEL
MIKOA ya Tabora, Katavi na Rukwa imetajwa kuwa ni miongoni mwa mikoa 10 inayoongoza kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011/2012 za Taasisi ya Mkapa.
Taarifa hiyo iliyotlewa na Meneja Mradi wa TB na Ukimwi kutoka Taasisi ya Mkapa, Dkt. Happenes Wilbroad   katika mafunzo ya siku moja ya viongozi wa dini yaliyofanyika  Nzega.
Alisema mkoa unaoongoza kwa maambukizi ya VVU kati ya mikoa hiyo mitatu ni Rukwa wenyeasilimia 6.2 ukifuatiwa na Katavi asilimia 5.2 na Tabora asilimia 5.1.
Dk. Wilbroad alisema Taasisi ya Mkapa  imeanza kuendesha  mafunzo ya kuhakikisha wananchi wanatambua na kuepuka maambukizi mapya.
Alisema   jitiahada mbalimbali za kudhibiti maambukizi hayo zinapaswa kufanyika  kunusuru maisha ya wakazi wa maeneo hayo.
Alitaja sababu zinazochangia   maambukizi kuwa ni pamoja na ndoa za utotoni, tohara za jadi na baadhi ya wananchi kutozingatia elimu ya Ukimwi   na kukithiri  imani potofu za ushirikina.
Wakizungumza baada ya mafunzo hayo, baadhi ya viongozi wa dini walisema watahakikisha wanashirikiana na serikali kwa kutoa elimu kwa jamii dhidi ya mapambano ya Ukimwi.
Mussa kassimu, Sheikh  wa mjini  Nzega  alisema elimu waliyopewa na wataalamu wa mafunzo hayo inalenga maagizo ya imani zao za dini hasa katika kukemea jamii dhidi ya mambo maovu.
Mchungaji wa Kanisa la AICT, Isaya lyaka,   AICT  alisema vitabu vya dini vinasema kila mmoja awe mwaminifu kwa mwenziwe  waliofunga ndoa na   kwa wale ambao bado wanapaswa kusubiri.