25.8 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

TABIA ZA WAZAZI HUCHANGIA KUHARIBU WATOTO

Image:

NA AZIZA MASOUD,

KATIKA ukuaji wa  watoto kuna tabia mbalimbali zinazojitokeza zinazoonekana na nyingine zinachlewa kuonekana kwakuwa zinajificha.

Zipo tabia za kurithi ambazo huwezi kuzizuia,ukiacha tabia za kurithi ambazo ni ngumu kumrekebisha wapo wenye tabia za kuiga.

Tania za kuiga  zinachangiwa na mtoto mwenyewe kupenda kuiga vitu vilivyopo katika  mazingira yanayomzunguka.

Kuna watoto wenye tabia za kuudhi wengine wanakuwa wacheshi ambao unatengeneza upendo kwa watu wanaomzunguka.

Mbali na hilo wapo watoto ambao hufundishwa tabia mbaya kwa makusudi  na watu wao wa karibu wapo ambao wanakuwa na tabia za kurithi kutoka kwa wazazi.

Tabia mbalimbali wanazokuwa nazo watoto kama za ukali,kuongea uongo,ukorofi,ulevi,kuvuta sigara na nyinginezo zinatajwa kusababishwa wazazi wanaofanya mambo hayo.

Kwa mujibu wa wataalam wa masuala ya saikolojia wanadai tabia za alizonazo mtoto huendana  na za  mzazi hivyo kuna haja wa wazazi kujichunga zao.

Hali ya mtoto kuwa mkali,mkorofi ni tabia ambazo zinatajwa kama za kurithi hivyo ni ngumu kuzimudu endapo mtoto husika atakuwa ajaamua.

Mzazi unapaswa kufahamu  mienendo na ya tabia zako zinaweza zikachangia kumuharibu au kuwaharibu baadhi ya watoto.

Ili kuweza kumuepusha mtoto kuingia katika tabia za ajabu unapaswa kuwa makini mfano   kama una tabia za kunywa pombe mbele  ya mtoto wako unategemea asinywe pombe anapokuwa mtu mzima.

Wapo wazazi ambao wanakuwa na tabia mbaya za kuwafundisha watoto wao kutumia vileo wakiwa wadogo kwakuwanywesha.

Mbali na vileo  wazazi wengine pia wabnashindwa kuwapa maneno mazuri watoto wanapokosewa badala yake  wanawafundisha kuwatolea maneno machafu ya kejeli wenzao tabia ambayo anakuwa nayo mpaka anapofikia umri wa utu uzima.

Wazazi tunapaswa kuwa makini katika malezi ili kuepusha watoto kuwa na tabia ambazo hazifai katika jamii inayotuzunguka.

Pia tuwe na tabia ya kuchunguza watoto zetu wanacheza na watoto wa namna gani na kujaribu kulinganisha tabia ya mtoto husika kama inaweza ikawa chanzo cha mtoto kujengeka vizuri kifikra.

Kumbuka tabia ama mwenendo wa mtoto unatengenezwa na mzazi husika,usitegemee mtu anaweza kutoka nje akamfundisha mtoto wako tabia nzuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles