26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Tabia ya vijana kuchagua kazi hukwamishamaendeleo yao

SHEILA KATIKULA, MWANZA

ELIMU ya ujasiriamali kwa wananchi ni jambo linalohitajika ili kuwaepusha vijana kukaa vijiweni bila sababu yoyote.

Hii ni kutokana na  kuwapo kwa changamoto ya ajira kwani kuna baadhi ya wahitimu kutoka vyuo mbalimbali huona aibu kujiajiri kwa kujiona kuwa  ni wasomi.

Hivi majuzi, nilimshuhudia mjasiriamali wa Kampuniya Agro Supplies kutoka wilayani Ilemela, jijini Mwanza, akionesha bidhaa mbalimbali ikiwamo kuuza sungura, miche ya maua, miti ya mbao, matunda, kufuga kuku na miche ya mboga mboga.

Mkurugenzi  wa Kampuni ya Kechu Agro Supplies, Kechu Nkya, huwa na desturi ya kufanya maonesho ya bidhaa mbalimbali mara kwa mara kwa lengo la kutoa elimu kwa watu ili waweze kupata ujuzi.

Nampongeza mama huyu aliyejitoa kwa miaka mitatu kuonesha kazi zake na bila kusaidiwa na mtu yeyote zaidi ya mumewe.

Vijana wengi licha ya kuwa ndio nguvu kazi, bado hawajitambui na hivyo hukaa bila kujishughulisha.

Nawashauri waige mfano huu ili kuimarisha ujuzi na ustadi wa kujiajiri wenyewe na si kusubiri kuajiriwa.

Kechu anasema wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujihusisha na shughuli za maendeleo kwa kuwa hadi sasawametoa mafunzo kwa watu zaidi ya 1000

Shule ya Msingi Laulenti ni miongoni mwa wale walionufaika na kampuni hiyo, baada ya wanafunzi zaidi ya 100 kupewa mafunzo yakupanda miche ya mboga za majani kwenye mifuko ya plastiki na ndoo, ili kuwaandaa waje kuwa wajasiriamali wazuri hatimaye wajikomboe na umaskini pindi watakapo hitimu masomo yao.

Niwakumbushe wakina baba kuacha tabia ya kuwafungia ndani wake zao na badala yake wawaache watoke kifungoni, wajishughulishe ili waweze kusaidiana majukumu ya nyumbani kwani kidole kimoja hakivunji chawa.

Utegemezi katika maisha si jambo zuri,  wanawake wajanja hujishughulisha na ujasiriamali.

Vijana nao wanapaswa kuacha tabia ya kuchagua kazi. Ili uweze kufanikiwa ni lazima kujitoa kwa hali na mali kuwekeza sehemu na si kukaa vijiweni bila sababu.

Familia nyingi huishi kwa shida kwa sababu ya kutegemea kipato cha baba tu. Utakuta mama na wanawe wote wamekaa nyumbani wakisubiri baba alete ndio wale, tabia hii itaendelea kuzifanya kaya nyingi kuishi kwa shida, ni vema wakabadilika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles