31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi zajitosa kurejesha uoto wa asili Mlima Kilimanjaro

Upendo Mosha, Moshi

Taasisi mbili zisizo za serikali, zimeanza harakati za kurejesha uoto wa asili katika Mlima Kilimanjaro kwa kuanzisha operesheni ya kupanda miti katika maeneo mbalimbali mkoani Kilimanjaro.

Taasisi hizo zinazojihusisha na masuala ya mazingira za Nipe Fagio na Borda Tanzania za Jijini Dar es Salam zimeanza mikakati hiyo kwa kupanda miti ya asili zaidi ya 250 katika Shule ya Sekondari Kimochi iliyopo Wilaya ya Moshi mkoani hapa.

Akizungumzia kampeni hiyo kwa niaba ya taasisi zote mbili, Ofisa Uhamasishaji wa Taasisi ya Nipe Fagio, Wilhard Shishikaye, amesema mbali na mradi huo kutekelezwa nchini Tanzania pia unatekelezwa katika nchini nyingine tatu duniani.

“Leo tumepanda miti hii ya asili 250 hapa na lengo letu ni kurudisha uoto wa asili katika mkoa huu hususani katika mlima Kilimanjaro ambao barafu yake imekuwa ikipungua siku hadi siku,” amesema.

Kwa mujibuu wa Shishikaye, nchi nyingine ambayo miradi hiyo inatekelezwa ni India, Brazil na Tanzania na kwamba mradi huo ulianza mwaka 2018 na unatarajiwa kumalizia mwaka 2020.

Awali akizungumza katika shughuli hiyo ya upandaji miti, mtaalumu wa miti kutoka Taasisi ya Kilimanjaro Project ambao ndiyo waratibu, Samuel Edrew, alisema miti yote inayopwanda husajiliwa kwa uratibu wa GPS ambapo huweza kufuatilia miti yote inayooteshwa.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kimochi, Crispine Njinjinji, alisema suala la mazingira ni nyeti na kwamba jamii inapaswa kubadilika na kucha tabia ya ukataji wa miti hovyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles