22.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi ys Mater Afrika yawapiga tafu Wajasiriamali Same

Na Safina Swartt, Same

Taasisi ya Kiraia ya Mater Afrika imewasaidia vijana na wanawake wanaotoka katika jamii ya kifugaji (wamasai) wilaya ya Same kwakuwapa elimu ya ujasiriamali pamoja nakuwapa mikopo isiyokuwa na riba kwa lengo la kuondokana na umaskini.

Mkurugenzi wa Asasi za Kiraia ya Mater dei Afrika, Mansuetus Setonga amesema juzi kuwa kuwa taasisi imeona umuhimu wa kuwasaidia vijana na wanawake wa kifugaji kutokana na jamii hiyo kuwa nyuma kimaendeleo.

Fr. Setonga amesema kuwa mpaka sasa vijana zaidi ya 30 wamepatiwa elimu ya ujasiriamali ili waweze kujiajiri na kutoa ajira kwa wengine.

Amesema kuwa mbali na kuwapatia elimu pia wanawapa mikopo isiyokuwa na riba ambapo wanakopeshwa kwa miezi sita na kurejesha ili wengine waweze kupata mikopo.

Amesema kuwa program hiyo ya kuwasaidia vijana ni moja ya maoni yake ya utumishi ivyo ataendelea kutoa huduma katika jamii.

Amesema taasisi hiyo pia imeweza kuwasaidia wanawake wa jamii za kifugaji (wamasai) kuwapa mashamba na mikopo ya kulima kilimo cha vitunguu, matikiti na nyanya.

“Tumewapa mashamba wanawake wa jamii za kifugaji (wamasai) na tumewapa na mikopo bila riba wakisha vuna mazao tunawatafutia soko,”amesema.

Nao baadhi ya wanufaika hao wameishukuru taasisi hiyo kwa kuona umuhimu wa kusawaidia wananchi wanaoishi mazingira magumu kujikwamua kiuchumi ili waweze kupata mahitaji muhumu ya familia zao.

Mmoja wa wanufaika hao, Rachel Athuman amesema kuwa taasisi Mater Afrika imewasaidia wanawake kujikwamua kiuchumi na kuondokana na hali ya utegemezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles