29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi ya TMEA kuisaidia Z’bar kukuza biashara

John Ulanga
John Ulanga

Na HARRIETH MANDARI, DAR ES SALAAM

TAASISI ya TradeMark East Afrika (TMEA), imeahidi kuisaidia Zanzibar katika kukuza biashara na kuondoa vikwazo vya biashara kwa bidhaa za Zanzibar, ili ziweze kuingia kwenye soko la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ahadi hiyo imetolewa na mkurugenzi wa taasisi hiyo tawi la Tanzania, John Ulanga,  alipokuwa akijibu ombi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) la kuisaidia Zanzibar kuondoa vikwazo vya kibiashara ambalo liliwasilishwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Balozi Amina Salum Alli.

Balozi Amina alisema ili kuisaidia Zanzibar kuepukana na vikwazo vya kibiashara kwa bidhaa kutoka huko kuingia katika masoko ya Tanzania Bara, soko la Afrika Mashariki na masoko ya kimataifa.

“Ili Tanzania ya viwanda ilete manufaa kwa Tanzania lazima viwanda viwafaidishe wananchi wa pande zote mbili za Muungano na jinsi gani Zanzibar itafaidika na Tanzania ya Viwanda.

“Jambo hilo huenda sambamba na bidhaa hizo kupata masoko ya kutosha ya kitaifa na kimataifa, ambayo yatahamasisha uzalishaji zaidi na kuvutia uwekezaji katika kujenga viwanda Zanzibar,” alisema Balozi Amina.

Akijibu maombi hayo, Ulanga alisema taasisi hiyo imepokea ombi hilo kwa mikono miwili ambapo itahakikisha inawaunganisha wafanyabiashara kutoka Zanzibar pamoja na kuwatafutia masoko ya uhakika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles