31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi ya Maendeleo Tengeru kuandaa viongozi wanawake

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

TAASISI ya Maendeleo ya Jamii Tengeru itaanzisha mradi wa kuandaa viongozi wanawake kutoka vyuo vikuu kwa lengo la kuongeza ushiriki wa wanawake na wasichana katika nafasi za uongozi.

Hayo yameelezwa leo Novemba 4,2022 jijini Dodoma na Mkuu wa Taasisi hiyo, Dk.Bakari George wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo na Mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka 2022-2023.

Mkuu huyo amesema lengo la kuongeza ushiriki wa wanawake na wasichana katika nafasi za uongozi

Amesema Taasisi inaendesha na kusimamia vituo viwili ambavyo ni Kituo cha Utafiti na Uhifadhi wa Machapisho yahusuyo Wanawake na Kituo cha Huduma Tandaa na Ubunifu wa Kidijitali.

“Taasisi inaendesha program 15 za mafunzo, kwa kipekee, mitaala inayotolewa na Taasisi imezingatia uwiano kati ya nadharia na vitendo.

” Hivyo mitaala yote inatekelezwa kwa kuzingatia dhana tatu ambazo ni uanagenzi, ushirikishwaji jamii na uanagenzi,”amesema Mkuu huyo.

Mkuu huyo amesema kwa mwaka 2021/2022, Taasisi ilianzisha Shahada ya Uzamili katika Usimamizi na Tathmini ya Miradi ambapo jumla ya wanafunzi 14 walisajiliwa kujiunga na Program hiyo.

Amesema katika mwaka 2022/23, udahili umeongezeka kufikia wanafunzi 25.

Aidha, kwa mwaka wa 2022/2023, Taasisi inatarajia kuongeza program 6 za mafunzo zinatarajiwa kuanza kutolewa dirisha la Machi 2023.

“Ambapo maandalizi ya program hizi yamezingatia mahitaji ya soko la ajira kwa sasa na umuhimu wa kuandaa wahitimu wenye fikra sahihi na uwezo wa kujiajiri,”amesema Dk George.

Dk. George amesema katika kipindi cha miaka mitano (2015/2016 hadi 2020/2021), Taasisi imetoa jumla ya wahitimu 2,350.

Amesema wahitimu hao baadhi yao wameajiriwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Mashirika yasiyo ya kiserikali na wengine kujiajiri wenyewe.

Mkuu huyo wa chuo amesema kwa mwaka 2022/2023, kituo kimepanga kufanya mkutano wa wadau wa masuala ya wanawake na kongamano la kitaifa la wanawake mwezi Machi 6 na 7, 2022.

Amesema kongamano hilo linatarajia kuwahusisha washiriki takribani 500.

“Tafiti 18 zinazoangazia masuala ya jinsia, ushiriki katika masuala ya uongozi zikitarajia kuwasilishwa,”amesema

Amesema kwa mwaka 2021/22, wasichana 15 kutoka vyuo vitano vya mkoani Arusha walidahiliwa chini ya programu hiyo.

Amema kwa mwaka 2022/23, wasichana 25 wanatarajiwa kudahiliwa.

Amesema kwa mwaka 2022/2023, kituo kinatarajia kushirikiana na wadau kutekeleza utolewaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwa kuzingatia falsafa ya maendeleo ya jamii.

Aidha, kituo kinaandaa programu ya mafunzo kwa maafisa bajeti wa mamlaka za serikali za mitaa kuwajengea uwezo katika maandalizi ya bajeti zinazozingatia usawa wa kijinsia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles