23.6 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Taasisi ya Alkhaibar Haji&Umraah yasafirisha mahujaji 16

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Taasisi ya Alkhaibar Haji&Umraah, imewasafirisha mahujaji 16 wanaokwenda Makka kwa ajili ya ibada ya hijja.

Mahujaji hao wameondoka leo saa tisa alfajiri katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA).

Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya mahujaji hao kuondoka, Mwenyekiti Msaidizi wa Taasisi hiyo, Khalid Sinani, amesema mahujaji hao watapewa huduma zote wakiwa huko na wanatarajiwa kurudi nchini Septemba 7, mwaka huu.

“Kila anayeenda hijja amelipia Dola za Marekani 3,800 ikiwa ni kwa ajili ya mahitaji yote yakiwamo chakula, mahema katika viwanja vitakatifu vya Makka na Arafa.

“Lakini mahujaji hawa pia wametoka maeneo mbalimbali ambapo kati yao kuna wanaume tisa na wanawake nane,” amesema.


Aidha, Khalid amesema wamesafirisha mahujaji wachache kutokana na mazingira  lakini walichofanya ni kutoa huduma na si biashara.

“Tunawatoa hofu Watanzania, taasisi hii ipo kwa ajili ya kusaidia Watanzania, mkombozi wa wanaokwenda katika ibada hiyo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,070FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles