24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi ya  Aga Khan yawezesha vikundi 90 zaidi ya Sh milioni 169

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Shirika la  Aga Khan Foundation  leo Juni 30, mwaka 2022 limetoa ruzuku ya Sh milioni 169,177,000 kwa vikundi 90 vya huduma ndogo za fedha lengo likiwa ni kuwainua wajasiriamali wadogo na kuwajengea uwezo ili waweze kuboresha biashara zao.

Kaimu Mkurugenzi Mkazi, wa Aga Khan Foundation, Simon Moikain, amesema ruzuku hizo wamezitoa kupitia mradi wanaoutekeleza wa  kuvisaidia vikundi vya huduma ndogo za fedha kutokana na changamoto za UVIKO-19 ambao unatekelezwa katika nchi tano ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Madagaska na Msumbiji.

Washiriki wa vikundi vya huduma ndogo za fedha mkoani Mwanza wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa hundi za ruzuku walizopewa na Shirika la Aga Khan Foundation lengo likiwa ni kuwainua wajasiriamali wadogo na kuwajengea uwezo ili waweze kuboresha biashara zao.

 Amesema mradi huo unafadhiliwa na  Shirika la  Aga Khan Foundation kwa kushirikiana na European uonion huku akifafanua kwamba hapa nchini unatekelezwa katika mikoa ya Mwanza Dar es Salaam, Mtwara na Lindi.

“Lakini katika kipengele cha ruzuku ya kuweka na kukopa kiko Mwanza katika halmashauri za jiji hilo, Buchosa, Ilemela,Magu na Sengerema, kwa mikoa mingine ni Lindi na Mtwara pekee, tunawezesha vijana, tunawafundisha masuala ya ujasiriamali na uwezo wa kusimamia biashara na wachache ambao wataonyesha ubunifu kwenye uandaaji na uendeshaji wa biashara,”amesema Moikain.

Mratibu wa mradi huo,  Japhet Wangwe amesema vikundi vyote vilivyopo kwenye mradi huo vitapata ruzuku ya zaidi ya Sh  Milioni 169 na vinaanza rasmi kazi kuanzia Juni 30 mwaka huu  na  kwamba mradi upo kwenye mfumo wa hisa ambazo zitaendeshwa kwa kutumia simu katika kufikia malengo.

Amesema mradi huo unafanya kazi na wajasiriamali hadi sasa wanao vijana 100 kutoka Mkoa wa Mwanza  ambao watajengewa uwezo wa kuboresha biashara zao ili waweze kujiinua na kuwaajiri  wenzao  ndani ya  jamii.

“Mhe Mkuu wa Mkoa tuliandaa utaratibu wa kupata vikundi hivi na tunashukuru ofisi za maafisa maeneleo za Halmashauri na Mkoa kwa usaidizi na hapa leo tupo na vikundi vya wawakilishi 90 ambavyo ndivyo vinaenda kupokea ruzuku hizi,” amesema Wange.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,  Mhandisi Robert Gabriel ametoa rai kwa vikundi vilivyofuzu kupata ruzuku hiyo  kwa ajili ya kuendesha biashara katika kupambana na athari zitokanazo na ugonjwa wa Uviko 19 kuzitumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kukithi  nia ya mradi huo.

“Kipekee kabisa naomba nimshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia awamu ya Sita  ya uongozi wake kwa kuendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na nchi mbalimbali ikiwemo Umoja wa Ulaya ambao pia wamefadhili mradi huu wakishirikiana na Shirika la Aga Khan Foundation.

“Hii ni fursa kubwa sana kwa mkoa kwa kupatiwa usaidizi wa kitaalamu na kifedha katika kuhakikisha wananchi wetu wanajengewa uwezo hivyo ni lazima mdhihirishe kwamba kule kuaminiwa kwenu kunaleta taswira kwamba  Mkoa wa Mwanza mradi ukileta unatekelezeka.” Mhandisi Gabriel,”amesema na kuongeza.

“Naomba niwasihi wanavikundi wote kuwa ruzuku hizi sio kwa ajili ya kufanyia sherehe, kununulia nguo mpaya  au kujengea nyumba, mnapewa fedha kwa ajili ya kuendesha biashara zenu katika kujiinua kutoka kwenye umasikini,”amesema Mhandisi Gabriel.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles