29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi Afya Aga Khan yaikabidhi Serikali Kliniki mbili za milioni 620

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Taasisi ya Huduma za Afya ya Aga Khan Tanzania (AKHS,T) imekabidhi Kliniki mbili zinazotembea zenye thamani ya Sh milioni 620 kwa Wizara ya Afya kwa lengo la kuboresha huduma za afya na kusaidia kupunguza upatikanaji wa huduma za afya hasa kwenye maeneo ya wafugaji na jamii za kuhamahama.

Kliniki hizo zitakuwa na jukumu katika kushughulikia tofauti za kiafya hasa kwenye maeneo yenye ufikiaji mdogo wa huduma za matibabu kwa jamii zilizokusudiwa.

Makabidhiano ya kliniki hizo ni sehemu ya mipango chini ya mradi wa chanjo wa ya Aga Khan COVID 19 unaofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani (KFW) kwa kushirikiana na Taasisi ya Huduma za Afya Aga Khan Tanzania (AKHS,T) na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya.

Akizungumza Jumatano,Novemba 8,2023 jijini Dodoma, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Serikali inawekeza kwa kiasi kikubwa katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora katika vituo vya afya vya ngazi ya chini na kati ili kupunguza adha ya magonjwa sugu.

“Serikali kupitia Wizara ya Afya inafuraha kubwa kupokea kliniki hizi zinazotembea kutoka kwa Washirika na wabia wetu. Kliniki hizi zimeundwa ili kutoa huduma za matibabu Shirikishi kwa kada mbalimbali katika watu walio katika mazingira ya wafugaji na jamii zinazohamahama,” amesema Waziri Ummy.

Amesema mradi huo unaonesha umuhimu wa kubuni miradi ambayo inachukuliwa kulingana na changamoto na mahitaji ya ndani.

Kwa upande wake,Afisa Mtendaji Mkuu wa Kanda ya Taasisi ya Huduma za Afya za Agha Khan,Afrika Mashariki, Dk. Zeenat Suleiman amesema malengo ya kimkakati ya AKHS,T ni kuendelea kuboresha mfumo wa utoaji huduma.

“Kujibu hili, mradi wa chanjo ya uviko 19 ulizaliwa,kupitia mradi huu, AKHS,T imeonesha dhamira yake ya kupunguza mzigo usio na uwiano wa magonjwa katika maeneo ya vijijini na watu ambao Wana changamoto ya kuzifikia huduma kwa urahisi.

“AKHST inashirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya na wadau kuboresha upatikanaji wa huduma za afya Bora kwa kutoa punguzo kubwa kupitia Mpango wa bima ya Afya (NHIF) wa kiasi Cha Sh bilioni 24,” amesema Dk. Zeenat.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles