23.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Taasisi 100 kushiriki kongamano la afya

Veronica Romwald, Dar es Salaam

Taasisi zaidi ya 100 zimethibitisha kushiriki kwenye kongamano la tano la afya (Tanzania Health Summit) ambapo jumla ya mada 40 zitawasilishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Novemba 12, Rais wa Kongamano hilo, Dk. Omary Chillo amesema asilimia 97 ya washiriki hao wanatoka ndani ya nchi huku asilimia tatu pekee wakitoka nje ya nchi ikiwamo Kenya, Uganda, Canada, Afrika Kusini, Burundi na India.

“Kongamano la mwaka huu linakuja na fursa mbalimbali kwa wadau wote walioko katika mfumo mzima wa afya nchini, viongozi, wawekezaji, watafiti na wabunifu watakutana kujadili mada kuu kuhusu dira ya Tanzania katika kuelekea uchumi wa viwanda,” amesema.

Amesema kauli mbiu ya kongamano hilo mwaka huu ni ‘Ukuaji wa Viwanda nchini Tanzania; Tathmini ya Ukuaji na Jinsi ya Kutatua Changamoto Zilizokithiri’.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo, Dk. Chakou Halfani amesema maandalizi yote yamekamilika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,184FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles