26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 21, 2024

Contact us: [email protected]

Synergy Tanzania yaipa tano Serikali kwa kutoa fursa kwa wafanyabiashara

Na Mwandiishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya Synergy Tanzania imeipongeza Serikali kwa kuendelea kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa madini nchini ili kukuza na kuendeleza sekta hiyo.

Hayo ameelezwa leo Oktoba 25, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Altaf Mansoor kwenye mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini 2023 alipotembelea kwenye mabanda mbalimbali yaliyopo kwenye mkutano huo.

Amesema hiyo ni fursa kwa wafanyabiashara ya madini kukutana na kujadili changamoto na fursa zilizopo kwenye sekta hiyo kwa maslahi mapana ya nchi.

“Serikali imetusaidia kutuletea fursa hii tunapaswa kuitumia kama ukiona peke yako uwezi tunaweza kuungana tukafanya biashara kubwa yenye tija na maslahi makubwa kwetu kama wafanyabiashara lakini pia nchi,” amesema Mansoor.

Ameongeza kuwa ukuaji wa sekta ya madini unachangia ongezeko la uchumi kwani ajira nyingi zinazalishwa na ulipaji wa kodi unaongezeka hali inayosaidia upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii ikiwemo shule, hospitali na miundombinu ya barabara.

Mansoor amesema kuwa ili kufanikisha shughuli za madini wafanyabiashara wanapaswa kushirikiana.

Amesema watanzania wanapaswa kutumia hizi fursa ili waweze kuwekeza kwani hata kama kwa kuungana lakini si kuziacha.

“Utendaji wa serikali unategea kwa kiasi kikubwa kodi zetu hivyo tunapaswa kuchangamkia fursa ambazo zitasaidia kuongeza ulipaji wa kodi,”a mesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles