25.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Sweden yamrudisha nyumbani balozi wake

STOCKHOLM, SWEDEN

SERIKALI ya Sweden imemrudisha nyumbani balozi wake nchini China kuhusiana na kuhusika kwake katika mkutano wenye utata uliohusisha binti wa muuza vitabu mwenye asili ya mataifa hayo mawili, ambaye anashikiliwa na China.

Balozi Anna Lindstedt, aliondoka Beijing juzi, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Sweden alisema.

Tukio lilianza kwa Angela Gui, ambaye baba yake, Gui Minhai anaaminika kutekwa na makachero wa China mwaka 2015, kuandika kwenye mtandao wa jamii kuhusu mkutano huo na Lindstedt.

Gui alikuwa mmoja wa wauza vitabu watano wa Hong Kong waliokamatwa. Vitabu wanavyouza vimekuwa vikiikosoa vikali China.

Gui, ambaye alisomea shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Cambridge  Uingereza, amekuwa akiendesha kampeni mitandaoni ya kutaka kuachiwa kwa baba yake.

Mwezi uliopita, Lindstedt alikaribishwa katika mkutano na kundi la wafanyabiashara wa China waliodai kuwa na ukaribu na Chama cha Kikomunisti cha China.

Gui alisema watu hao walimshinikiza akubali kuingia makubaliano  ambayo yatamfanya aache kuzungumza hadharani kuhusu kesi ya baba yake na kumuahidi angetumikia kifungo cha miaka mitano na   kuachiwa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sweden ilisema haikupewa taarifa za kuwapo mkutano huo uliohudhuriwa na Lindstedt, ambaye kwa sasa anakabiliwa na uchunguzi wa ndani.

Kwa mujibu wa Gui, Lindstedt aliwasiliana naye na kusema kuna mbinu mpya kuhusu kesi ya baba yake na kumtaka ahudhurie mkutano na wafanyabiashara hao mjini Stockholm,” Gui aliandika mtandaoni.

Akapanda ndege kuelekea Stockholm na kufikia katika hoteli waliyopanga kukutana, ambako alipelekwa kwenye ukumbi alikoonana na watu hao.

“Kulikuwa na vinywaji vingi vya kulevya na maswali mengi ya ajabu ajabu,” Gui aliandika.

“Lakini kwa sababu Balozi Lindstedt alikuwapo na alionekana kuridhika na kila kinachoendelea, nikadhani ni mkutano ulioandaliwa na wizara ya mambo ya nje ya Sweden.”

Anasema mmoja wa wafanyabiashara alimpa ofa ya kufikia makubaliano  ambayo baba yake angeenda mahakamani na kufungwa jela miaka michache ili binti aache kuandika hadharani kuhusu kushikiliwa kwa baba yake.

Kwa mujibu ya maelezo ya Gui, Lindstedt alionekana kuunga mkono mpango huo, akimwambia kuwa China inaanzisha mpango mpya wa  diplomasia na iwapo ataendelea kutoa matamko mitandaoni China inaweza kuiadhibu Sweden.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,211FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles