Surua yaua mara mbili ya ebola Congo

0
769

KINSHASA, CONGO

UGONJWA wa Surua umewaua takriban watoto 5000 katika taifa la Jamhuri ya KidemokrasIa ya Congo mwaka huu wa 2019, baada ya ugonjwa huo kusambaa katika mikoa yote.

Kulingana na taarifa za mamlaka ya nchi hiyo takriban watoto 250,000 wameambukizwa mwaka huu pekee.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa ugonjwa huo ndio janga linalosambaa kwa kasi mno.

Ugonjwa huo wa surua nchini Congo umeua idadi ilio mara mbili ya wagonjwa waliofariki kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola katika kipindi cha miezi 15 iliopita.

Serikali ya Congo kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani (WHO) imezindua chanjo ya dharura mwezi Septemba inayowalenga watoto 800,000.

Lakini miundo mbinu mibaya, mashambulizi dhidi ya vituo vya afya, mbali na ukosefu wa tiba za mara kwa mara zimekwamisha juhudi za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.

Watoto milioni nne tayari wamepewa chanjo, lakini wataalam wameonya kwamba idadi hiyo ni chini ya nusu ya jumla ya watoto nchini humo na kwamba chanjo zilizopo hazitoshi.

Wengi walioathirika na ugonjwa huo ni watoto wachanga.

Surua ni virusi vinavyosababisha mtoto kuwa na mafua kutoa vipele vidogovidogo ambavyo vinaanza usoni na kusambaa mwilini na  kuwa joto kali.

Wengi hupona, lakini surua inaweza kusababisha ulemavu wa muda mrefu. 

Inaweza kusababisha kifo hususan iwapo utasababisha homa ya mapafu ama uvimbe katika ubongo.

Inakadiriwa kwamba jumla ya watu 110,000 duniani hufariki kutokana na ugonjwa huo kila mwaka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here