32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

SURA TATU ZA UTEUZI WA POLEPOLE ITIKADI NA UENEZI CCM

humphrey-polepoleDESEMBA 13, 2016, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilitoa taarifa kwa umma juu ya mabadiliko ya muundo wa chama hicho pamoja na kutoa taarifa za uteuzi wa nafasi mbalimbali ikiwano nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho.

Katika akaunti yake ya Twitter, CCM ilisema kuwa “Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kimemteua  HYPERLINK “https://twitter.com/hpolepole” Humphrey Polepole kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi.”

Kwa siku ya leo sitachambua mabadiliko ya muundo yaliyofanywa lakini nitajielekeza katika uchambuzi wa nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo.

Binafsi ninautafsiri uteuzi wa Polepole kwa namna tatu. Namna ya kwanza ni nafasi ya Polepole katika utetezi wa Katiba ya Wananchi iliyowasilishwa ndani ya Bunge Maalumu la Katiba na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba, Katiba ambayo wana CCM waliizika rasmi na kuibuka na rasimu yao mpya ya Katiba inayopendekezwa!

Namna ya pili ni kazi ngumu aliyonayo Polepole ya kubadilisha mtazamo wake ili aendane na mtazamo wa chama chake CCM ambacho kilikataa rasimu ya Katiba ya Wananchi iliyopendekeza muundo wa Serikali tatu na kuamua kubakia na rasimu ya Katiba inayopendekeza muundo wa Serikali mbili.

Hapa Polepole ana kazi kubwa; ni ama yeye awashawishi wana CCM wenzake kukubaliana na muundo wa Serikali tatu kazi ambayo najua hataweza au yeye akubali kutotia kitumbua chake mchanga kwa kuamua kubakia na cheo chake kipya na kuungana na msimamo wa chama kuwa na muundo wa Serikali mbili.

Namna ya tatu ni kuwa kwa maoni yangu nauona uteuzi wa Polepole kama ujumbe wa Mwenyekiti wa CCM kuwa anakubaliana na muundo wa Serikali tatu na mchakato wa kura ya maoni (referendum) juu ya rasimu inayopendekezwa unaweza usiendelee na badala yake mwenyekiti wa CCM akishawishiwa na watu kama akina Polepole watarejesha rasimu ya Jaji Warioba ambayo kimsingi ndiyo  wananchi wanaitaka.

Kuhusu namna ya kwanza tayari Polepole ameshaanza kuongea kuwa CCM itarudi kwenye misingi yake. Katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii, Polepole Desemba 19, 2016 aliandika kuwa “Tunarudi kwenye misingi”. Hii inaonesha kuwa mtazamo wa Polepole juu ya CCM ya sasa ni kuwa CCM ilipotoka na kuiacha misingi yake! Lakini pia katika mtazamo huu ni wazi kuwa kijana mwenzetu huyu haridhishwi na hali ya mambo ndani ya CCM kama ilivyo hivi sasa.

Kwa hiyo sisi huku mtaani tunamtarajia kijana mwenzetu huyu akiwa ndani ya vikao vya maamuzi vya CCM basi aitetee Katiba ya Wananchi kama alivyokuwa akiitetea kabla ya kushika wadhifa huo mpya.

Kwa uwepo wake ndani ya nafasi hii nyeti ndani ya CCM sitarajii mchakato wa kura ya maoni kuendelea kwa kuwa Katiba inayopendekezwa si ile aliyokuwa akiipigania kabla ya nafasi yake mpya ndani ya chama.

Tunamtarajia Polepole amshawishi mwenyekiti wa CCM kuamini kuwa njia bora na sahihi ya kuinyoosha nchi hii ni kuamua kuirejesha rasimu ya Katiba ya Wananchi. Pia tunatarajia ndugu yetu huyu awaambie ukweli CCM kuwa wananchi wanataka Katiba yao inayotaka uwepo wa Serikali tatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles