25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Sungusungu wachoma vibanda 100 vya wakulima, wavuvi

Walter Mguluchuma -Katavi                          

 ZAIDI ya vibanda 100 vya kuishi wavuvi na wakulima vimechomwa moto na sungusungu katika Kitongoji cha Masogangwi, Kata ya Itenka, Halmashauri ya Nsimbo, Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi na  kusababisha uharibifu wa mali za thamani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari  na  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga, tukio hilo lilitokea jana saa nane mchana katika kitongoji hicho.

KuzagaaAlisema kabla ya tukio hilo, Mtemi wa sungusungu  wa  Kijiji cha Tumaini, Halawa Ligoba, alifika kwenye kambi hiyo kisha kuwakusanya wakazi wa eneo umbali wa mita 100 kutokea kwenye vibanda vyao.

 Ilidaiwa wananchi hao walielezwa wanakusanywa eneo hilo ili mtemi huyo afanye nao mkutano wa hadhara.

 Kamanda Kuzaga alisema baada ya kukusanywa ndipo  kikundi cha sungusungu kinachoongozwa na mtemi huyo, kilifika eneo hilo huku wakiwa na silaha za jadi na kuanza kuchoma zaidi ya  vibanda 100 vya makazi ya watu hao.

 Alisema sungusungu walikaa eneo hilo hadi walipohakikisha vibanda hivyo vilivyoezekwa kwa nyasi vimeteketea kwa moto ndipo walipoondoka.

Kuzaga alisema polisi walipata taarifa ya tukio hilo na walifika eneo hilo na  kuwakamata watuhumiwa wawili.

 Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Bujima  Maginya (50)  mkazi wa  Kijiji cha Tumaini na  Shalu Charles (32)  mkazi wa Kijiji cha Kakese ambao bado wanaendelea kuhojiwa na Jeshi la Polisi huku watuhumiwa wengine wakiendelea kusakwa.

 Kamanda Kuzaga alisema chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

 Alitoa wito kwa wananchi wenye tabia ya kujichukulia sheria mkononi kufanya vitendo vibaya  ndani  ya jamii vya uvunjifu wa amani kuacha mara moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles